Stori kutoka kwenye bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania July 26 2012 ni kuhusu Swali alilouliza
Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Swali la Mchungaji lilitokana na taarifa kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa tamko kuwachukulia hatua wananchi watakaoonekana wanakula mchana au kuvaa nguo fupi wakati wa mfungo wa Ramadhani.
Mch Msigwa alimuuliza Waziri mkuu “Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nimesema haina dini, je ni wakati muafaka kwa Serikali yako kutangaza sasa kwamba upande mmoja wa Muungano una fuata sheria za kidini na upande mwingine wa Muungano hauna dini?
Kauli aliyoitoa Waziri mkuu kumjibu mchungaji Msigwa ni hii…. “Nasema hili kwa maana ya mazingira ya Zanzibar, ukienda Zanzibar tungechukua tu takwimu za jumla jumla unaweza ukaona kabisa karibu asilimia 99 hivi ni Waislamu, sasa ndio maana nasema kwa mazingira ya Zanzibar viko vitu ambavyo vinaweza vikafanyika na mimi nadhani kwa sehemu kubwa atakua alipima vilevile mazingira, usilifanye likawa jambo kuuuubwa, angekua anazungumza kwamba serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ofcourse ingekua tofauti”

6 comments:
Huyo mchungaji yeye aendelee kuchunga kondoa wake huko barabara, waziri mkuu kamjibu sawa sawa, muwadanganye huko huko bara, mmewavuruga uislam bara, mmewakandamiza waislam, sasa mnataka kuja kutuvuruga na huku?
Na dini mnazo na serikali inadini vile vile, si kama hivyo wewe mchungaji unaitumikiaje nchi ya kikafir isiyokuwa na dini? Mnamdanganya nani, na kama nchi haina dini huyo mnayemuombea kila siku nani na mnamuomba nani?
takwimu za uislamu tunazipata wapi? maana hata kwenye sensa swala la udini wa mtu halikuwekwa kwenye takwimu, pili kuna watu wasiyo waislamu huko watalazimishwa kufunga kwakuwa waislam wamefunga?
Hiyo sheria haiwahusu watalii kutoka nje ya nchi (wazungu) Hakuna mzungu anayeweza kukamatwa kutokana na ukiukwaji wa sheria hiyo. African Americans and black Europeans itabidi wawe makini kidogo na hilo, vinginevyo wanaweza kukamatwa na kuachia baada ya kujitambulisha.
Na mimi naongezea kuhusu suala hili. Zanzibar wana utaratibu wa aina hii tokea kabla ya uhuru hadi uhuru wake. Namuomba mchungaji assome historia ya nchi hizi mbili.
Nchi kutokuwa na dini maana yake ni kwamba serikali haiamini katika dini yoyote kwa maana ya taratibu lakini watu wake wana dini na imani mbalimbali hata uchawi. Ni dhaha ya secular state. Nenda shule ukajifunze mambo haya siyo kutoa tu maoni kwa kuwa una kompyuta.
Lakini pia huwezi kumlazimisha muumini kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu. Mwache mtu na imani yake; kwa nini serikali au shehe amfundishe mtu kumtii Mola wake?
Ni wapi ambapo Alla amesema kwamba wanadamu wamsaidie kuwatia adabu wanadamu wenzao? Ndiyo haya haya yanayotufikisha kwenye ugaidi.
Mimi Muislamu na sifungi kwa sababu zangu binafsi; sasa kwa nini mnilazimishe? Nakwenda Zanzibar wiki ijayo na hamnifanyi kitu chochote.
Juma Mbizo.
namungu mkono mdau wa mwanzo aende kawa chunge kondo wake huko huko bara siyo visiwani hata haya haoni mwezi mtukufu huu ra ramadhani anataka kutuleta zake za kuleta kama mchungaji mbona yuko mwanasiana na kama nchi haina dini mbona yeye ame pewa power ya kusema haya kawadanganyeni huko huko watu wenu wa bara sisi tumeshaamka huku long long time kwa ufisadi wenu, mtatuuwa lakin inshallah kuna siku tutaipata zanzibar yetu huru yenye mamlaka yake siyo mkoo huu ilipojingua na tanganyika ilikuwa ni nchi tafuteni nchi yenu Tanganyika mwalimu kaiuwa kwa nini muulizeni.
mchungaji nenda kachunge kondoo wako bwana usitulete za kuleta sawa shika lako la zanzibar tuachiye tufunge kwa salaam mwezi wetu mtukufu huna hata haya wee unamuabudu kweli yesu mbona vitendo vyako viko tafauti na vya yesu
Post a Comment