ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 16, 2012

ELIMU JUU YA SENSA YA TAIFA


Tawi la DMV
P.O.BOX 56356 WASHINGTON DC 20040
 Email address:ccmwashdc@gmail.com

16 July,  2012

TAARIFA KWA WANANCHI JUU YA ZOEZI LA SENSA YA TAIFA-2012


Watanzania wenzangu kama tunavyofahamu mwaka 2012 ni mwaka ambao nchi yetu inafanya zoezi maalumu la sensa ya taifa. Sensa hii inafanyika kila baada ya miaka kumi, sensa ni zoezi maalumu linalofanya na serikali ili kuesabu watu na makazi, na lengo lake ni takwimu sahii zitazopatikana katika zeozi hili zitumike katika taratibu maalumu za mikakati ya serikali kupanga utaratibu wa maendeleo kwa wananchi wa nchi yake. Mfano, mimi ni miongoni mwa watanzania waliobahatika kuhusika katika sensa ya marakani iliyofanyika miaka michache iliyopita chini ya idara ya takwimu, wizara ya kazi na ilikuwa elimu ya mafunzo kama mwanafunzi ( internship). Kwahiyo si vibaya kutumia muda huu ili kueleza kile kidogo nilichoweza kujifunza katika zoezi hili watanzania wenzengu waweze kufaidika na umuhimu wa zoezi hili.


Utangulizi

Zoezi la sensa ya taifa litafanyika mwezi wa August 25 kuamkia 26 mwaka huu 2012.
Zoezi hili linasimamiwa na Idara ya ofisi ya Takwimu, chini ya wizara ya fedha. Idara hii inaongozwa na Dk. Albima Chuwa. Tanzania chini ya idara hii ya takwimu inatumia technologia ya kisasa iitwayo Optcal Mark reader kwa maarufu ni ufundi wa scanning wa kitechnologia ambao ni nchi chache katika bara la Afrika wanazotumia. Zoezi hili la sensa lilifanyika mwaka 2002 na liliweza kufanikiwa kwa kiwango cha juu na kuzifanya baadhi ya nchi nyingi barani la Afrika kuja nchini Tanzania kujifunza katika miaka hii michache juu ya mafanikio yaliyopatikana na idara hiyo ya takwimu ya serikali. Mfano wa nchi ambazo wameweza kujifunza na kufuata taratibu hizi kwenye idara ya takwimu ni Ghana, Angola, Sudan,Ethiopia, Elitrea na Lesotho. Si hivyo tu, kutokana na Tanzania kuwa na mfumo ambao ni imara na wakuweza kutoa taarifa za takwimu sahii za zoezi hili ukilinganisha na nchi nyingine katika bara la Afrika, Tanzania imeweza kuwa mjumbe wa kamisheni ya takwimu ya umoja wa mataifa kwa muda wa miaka minne kuanzia january 2012 na sababu kubwa iliyotokana na umairi na ukufuzi, usimamizi na mafunzo yanoyotolewa katika ngazi ya taifa, mkoa, wilaya, kata na makarani wa zoezi hilo na kufanikisha kutoa takwimu sahii ukilinganishwa na nchi nyingine barani afrika. Kama tunavyofahamu sensa hufanyika na mataifa mbali mbali duniani. Tanzania inafuata mfumo wa kufuata kanuni, taratibu na miongozi uliwowekwa na umoja wa mataifa.


Nini maana ya sensa ?

Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa serikali wa kukusanya, kuchambua , kutathmini na kuchapisha au kusambaza takwimu za kidemografia ,kuichumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu ( kawaida ni miaka kumi). Kwa maana nyingine ni zoezi maalumu linafanywa na serikali lenye utaratibu ambao unakusanya taarifa za idadi ya watu na makazi na kuzitumia takwimu hizo za taarifa kuweza kutathimini ubora wa hali ya maisha ya watanzanzia na kuiwezesha serikali kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wake.

Nini lengo la sensa?
                                                     
Lengo la zoezi la sensa litaiwezesha serikali kuwa na takwimu sahii kuhusiana na watu ambazo zitachangunua na kuainisha kwa makundi, ukubwa, mtawanyiko au msongamano wa watu na makazi katika maeneo yote ya nchi. Vile vile, taarifa za sensa zinaweza kuisaidia serikali katika kupanga na kutekeleza mipango yake ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mfano, takwimu hizi zinazotokana na zoezi la sensa zinaisaidia serikali kujua mahitaji halisi ya wananchi wa Tanzania yakiwemo makundi yenye mahitaji maalumu, mathali ya watu wenye ulemavu, na kuiwezesha serikali kuwa na mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu. Kwahiyo madhumuni makuu ya sensa ya taifa ni kujua idadi ya watu na makazi nchini pamoja na kukusanya taarifa zao muhimu kama vile umri, jinsia, mahali wanapoishi, hali ya ndoa, kiwango cha elimu, hali ya ajira, hali ya uzazi na vifo, hali ya makazi na taarifa nyinginge muhimu kwa maisha yao ya kila siku.

Si, mara ya kwanza Tanzania kufanya zoezi hili la sensa, sensa iliweza kufanyika katika miaka ya 1967, 1978,1988, na 2002. Kama nilivyotangulia kusema mwaka huu 2012 sensa itafanyika August 26. La kutia moyo miaka hii ya karibuni limeweza kufanyika kwa ufanii zaidi. Na ndiyo maana ripoti za kimataifa zinaonyesha Tanzania katika kipindi cha miaka kumi kumeweza kupiga hatua katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii. Mfano, kutokana na taarifa ya benki ya dunia inoenyesha Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeweza kufanikiwa kuwa na mikati imara ya elimu kwa wananchi wake, huduma ya afya na sekta mbali mbali za uchumi kama vile kilimo na kuifanya nchi kukuza uchumi wake  kwa asilimia 6.7 kwa mwaka  ikilinganishwa na nchi nyingine duniani kama vile china na india, kutokana na taarifa sahii za takwimu zilizoweza kupatika katika sensa ya 2002.

Kama tunavyofahamu malengo makubwa ya mikakati ya kuuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) kwa upande wa Tanzania bara ni kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa kipato, kuinua kiwango cha maisha na ustawi wa jamii na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji. Na kwa upande wa Zanzibar mpango huu unajulikana kama  MKUZA wenye malengo matatu:
1.       Ukuzaji wa uchumi
2.       Ustawi wa jamii ulio bora
3.       Ujenzi wa misingi ya utawala bora
Hivyo basi tunaimani kabisa taasi husika litalifanya zoezi hili kufanyika kwa ufanisi zaidi kama lilivyoweza kufanyanyika mwaka 2002. Kutokana na Uzoefu wangu wa Intership ya zoezi hili nilioupata hapa marekani, tungeweza kuishauri mamlaka husika kuendelea kutoa mafunzo maalumu katika ngazi zote za taifa, mikoa, wilaya, kata na makarani. Kuweza kuakikisha vifaa muhumu vya kitechnolojia vinasambazwa kwa muda muafaka bila kuchelewa. Vile vile, wahusika wakubwa katika kutoa taarifa kama vile walimu, wenyeviti wa vijiji na wahusika wakuu kutoa taarifa zilizo sahii.
Wito kwa wahusika kufanikisha zoezi hili
Kwahiyo tunatoa wito kwa vyombo vyote vya habari magazeti mbalimbali, redio, vituo vya televisions,blogs na websites mbali mbali watumie fursa hii kuwaelimisha watanzania ni nini maana ya sensa na malengo yake.  Wito kwa wadua mbali mbali kama vile, viongozi wa wa umini wa dini ya kikristo, kiislamu na watu wa madhehebu mbalimbali kutumi kipindi hiki kifupi kuelewesha watanzania umuhimu wa zoezi hili. Kwa wale wadau wa vyuo na wanasanaa watumie fursa hii kwa kutumia ngojera, kwaya , mashairi na ngoma na utamaduni wa mtanzania kwa lengo la kuilewesha umma juu ya umuhimu wa zoezi hili. Tunamatumaini makubwa wa wahusika wa maeneo muhimu wa utoaji habari muhimu katika sensa kama vile hospitali, vyuo, shule , kambi za jeshi, kambi za wakimbizi, nyumba za kulala wageni na magereza mmejipanga vizuri katika zoezi hili. Nimatumaini yangu zoezi la sensa ya Taifa la mwaka 2012 litafanyika kwa ufanisi zaidi bila wasiwasi  ili taarifa mbali mbali kama vile shule,, vyuo, hospitali, vituo vya afya, zahanati, masoko, huduma za fedha, majosho, vyanzo vya maji, miundo mbinu kama vile barabara, madaraja na mawasiliano zitazopatikana zitakuwa sahii. Hivyo taarifaa itakayopatikana katika zoezi hili la sensa litaweza kuisaidia serikali kutimiza malengo yake ya kupanga mikakati ya maendeleo kwa watanzania kama vile mikakati ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa kupunguza umaskini wa kipato, kuinua kiwango cha maisha na ustawi wa jamii kwa kuboresha humuma muhimu za watanzania kama vile elimu, na afya. Na mpango, kutimiza mpango muhimu wa serikali wa 2015 wa mpango wa maendeleo ujulikanao Milenium.
Mwisho, tunawatakia watendaji wote wa serikali mafanikio mema ya utendaji katika zoezi hili muhimu la serikali kuanzia idara ya takwimu za taifa, mikoa, wilaya, tawi na watendaji. Rekodi inaonyesha zoezi hili lilipofanyika mwaka 2002 lilifanyika kwa ufanisi wa viwango vilivyowekwa na umoja wa mataifa na kuweza kuitangaza Tanzania kuwa mwalimu wa mafunza wa nchi nyingine barani afrika kama vile Ghana, Angola, Sudan, Ethiopia, Elitrea na lesotho.
Kwaniaba ya watanzania waishio nje ya nje, tunatoa pongezi kwa kulitumikia taifa letu changa na lenye bajeti ndogo na mazingira magumu ya kazi. May god bless you
Mungu ibariki Tanzania

Asanteni
Katibu wa Tawi CCM Washington DC
Yacob Kinyemi

4 comments:

Anonymous said...

Hongera sana kiongoz wangu maelezo yanajitosheleza by cleopa nzogera

Anonymous said...

Elimu ya sensa

Anonymous said...

Thank

Anonymous said...

Thank you