ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 25, 2012

HIVI NDIVYO MWANZA TSC WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA BAADA YA KUIFUNGA STUTTGART




MJERUMANI JURGEN - MRATIBU WA SAFARI YA TSC NCHINI GERMANY

Huyu ndio mratibu wa safari nzima ya kituo cha TSC Mwanza kuja hapa Ujrumani, anaitwa Bwana Jurgen. Amefurahishwa sana na ushindi wa vijana wa TSC dhidi ya Stuttgart na akadiriki kusema anaona wachezaji wa TSC wana potential ya kufanya vizuri sana kwenye careers zao za soka.

MWALIMU WA TSC MWANZA - ROGISIAN KAIJAGE AWASIFU VIJANA WAKE KWA KUTWAA KOMBE



MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA ASHUHUDIA TSC WAKIBEBA UBINGWA UJERUMANI



TSC MWANZA YAIFUNGA TIMU BORA YA VIJANA NCHINI UJERUMANI NA KUBEBA KOMBE

Kikosi cha TSC kilichochukua ubingwa kwa kuifunga Stuttgart.

Ziara ya timu ya kituo cha TSC Mwanza nchini Ujerumani imeendelea leo kwa kushiriki kwenye michuano mifupi ya 1 ya kombe la Brackenheim-duerrenzimmern iliyoshirikisha timu 3, ikiwemo klabu bingwa ya Bundesiliga under 19 mara 10, klabu ya Stuttgart ya hapa Ujerumani.


Kwenye michuano hiyo iliyoanza mida ya asubuhi hapa Ujerumani, timu ya kituo cha TSC Mwanza iliifunga klabu ya Statauswahl kwa bao 2-1, magoli yakifungwa na Tito Jonas na Japhet Vedastus, kabla ya jioni kucheza yake ya mwisho dhidi ya mabingwa wa mara 10 wa Bundesiliga under 19, klabu ya Stuttgart na kufanikiwa kuifunga kwa mabao matatu kwa mawili.

Kikosi cha Stuttgart kilichoanza leo dhidi ya TSC.
Magoli ya TSC yalifungwa na Miraji Madenge 'Shevchenko',  Japheti Vedastus akaongeza la pili,  kabla ya Stuttgart kusawazisha yote mawili, lakini alikuwa yule yule Miraji Madenge  aliyepachikwa jina la utani 'Shevchenko' akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Stuttgart na kuiwezesha timu yake kubeba ubingwa wake wa kwanza tangu kufika hapa Ujerumani.
Benchi la ufundi la TSC Mwanza

No comments: