Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara
hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13,
WABUNGE vijana walioko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
watapaswa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria
kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2012/13.
Waziri wa Ulinzi na JKT, Shamsi Vuai Nahodha alisema hayo alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya wizara yake bungeni jana. Alisema wabunge vijana watakuwa sehemu ya kundi la kwanza la vijana 5,000 katika mafunzo yatakayoanza Machi, mwakani.
Alisema wizara hiyo imelifanyia kazi ombi la kuandaa mafunzo ya JKT kwa wabunge vijana kama ilivyoombwa mwaka jana na kwamba wabunge hao wameandaliwa mafunzo hayo ya wiki tatu.
“Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Wizara yangu imelifanyia kazi ombi hilo na kuandaa utaratibu wa mafunzo maalumu ya wiki tatu kwa waheshimiwa wabunge vijana,” alisema Nahodha na kuongeza:

No comments:
Post a Comment