ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 10, 2012

GLOBAL PUBLISHERS YAZINDUA SHINDANO LA ‘JISHINDIE NOAH’


   Meneja wa Global Publishers,  Abdallah Mrisho (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Kushoto kwake ni Ofisa Tarafa wa Magomeni, Flugens Lisakafu, Mhariri Mtendaji wa Global, Richard Manyota na Mratibu wa shughuli mbalimbali za Glabal, Juma Mbizo.
Lisakafu (katikati) akizungumza katika hafla hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) akiipongeza Global Publishers kwa hatua yake hiyo ya “kuwakumbuka” wasomaji na wananchi kwa jumla. Kushoto ni Abdallah Mrisho na kulia ni Richard Manyota
Abdallah Mrisho akionyesha mojawapo ya simu aina ya Samsung Galaxy ambazo zitashindaniwa sambamba na Noah hiyo.
Kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally na kulia ni Bw. Lisakafu.
 Bw. Lisakafu akifungua mlango wa gari aina ya Noah linaloshindaniwa.
...Akizindua shindano hilo.
Gari aina ya Noah linaloshindaniwa.
Picha ya pamoja ya baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo.
KAMPUNI  ya Global Publishers ambayo huchapisha magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, leo imezindua rasmi shindano la ‘Shinda Noah’ katika ofisi zake zilizopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar.


Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo wa uzinduzi, Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho, amesema huo ni utaratibu ambao kampuni imejiwekea kurudisha sehemu ya mapato kwa wateja wake na  kama ilivyokuwa kwa miaka mitano iliyopita, mwaka huu gari aina ya Noah litatolewa.

“Mbali na zawadi hiyo ya gari, zawadi nyingine ambazo ni  simu za mkononi, televisheni, na nyingine kibao zitatolewa kwa wasomaji wa magazeti pendwa na kwa kutuma kuponi kwa anuani elekezi,” alisema Mrisho.

Mgeni rasmi katika promosheni hiyo inayoanza mwezi huu wa Agosti na ambayo itafikia kikomo mwezi Novemba, alikuwa ni Ofisa Tarafa wa Magomeni, Flugens Lisakafu., ambaye alifika kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Lugimbana.

PICHA/PICHA : ERICK EVARIST NA RICHARD BUKOS / GPL

No comments: