ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 22, 2012

RISASI ZA MOTO ZATUMIKA KUTULIZA GHASIA KATIKA ENEO LA KARIAKOO


Nyumba inayolalamikiwa ikianza kuvunjwa

Kijana akiburuzwa kama mzoga maisha ya nyumbani hayo

 Askari Polisi akiweka mabomu ya machozi katika bunduki yake huku akiangalia hali ya usalama wake.

DAR ES SALAM, Tanzania


RISASI na mabomu ya kutoa machozi leo vilirindima katika maeneo ya Kariakoo baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba kwa zaidi ya miaka 40 akidai kuwa ni yake.

Hali hiyo imekuja baada mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said kushinda kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo mahakama ili mtaka mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Shaban Hassan kuondoka katika nyumba hiyo.

Akizungumza katika eneo la tukio kiongozi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Isaac Nguku alisema walifika eneo hilo kwa amri ya Mahakama kwa lengo la kukabidhi nyumba hiyo kwa Said.

Amesema kuwa hata hivyo, walipofika katika eneo hilo majira ya saa 5:00 asubuhi walikuta kundi la vijana ambao inasadikika kuwa waliandaliwa na Hassan kwa ajili ya kukwamisha zoezi hilo.

Nguku alisema baada ya kuona hali hiyo waliamua kuomba msaada kutoka polisi ambapo walifika na kuanza kuwatawanya vijana hao.

“Vijana hao hawakuridhika ndipo wakaanza kuturushia mawe kutoka kila kona walizokuwa wamejipanga kitendo hicho kilisababisha askari kufyatua risasi za moto juu huku wakipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya mbali” alisema Nguku.

Baada ya vijana hao kutawanyika mitaa minne inayozunguka nyumba hiyo ilifungwa, mitaa hiyo ni pamoja na Kongo, Mkunguni, Tandamti na Mchikichini

Naye mmiliki wa nyumba hiyo, Said alisema wavamizi hao walipanga katika nyumbani hiyo tangu mwaka 1972 ambapo baada ya hapo wakajitengezea hati bandia kwa lengo la kumdhulumu mama yake mzazi.

Alisema kitendo hicho kiliwafanya wafikishe kesi hiyo mahakamani ambako waliwakilisha hati zao ambazo zimewafanya washinde kesi hiyo, mvamizi huyo  kuamriwa aondoke kitendo alichokipinga huku akikata rufaa za mara kwa mara lakini hata hivyo akawa anashindwa mara zote.

Nyumba hiyo inayogombewa iko mtaa wa Karikoo kitalu namba 86, hata hivyo wakati zoezi hilo likiendelea mvamizi huyo alikuwa  ndani kwa ajili ya kutumikia kifungo cha siku 21 kwa picha zaidi ya tukio hili bofya read more. na tunaomba radhi kwa picha hizo 



 Majerui katika vurugu hizo
 Baadhi ya vijana waliokamatwa katika vurugu hizo wakiwa katika gari la Polisi lenye namba za usajili T 220 AMV
 Kijana aliyekaidi amri ya Polisi wakati akipita katika eneo lililokuwa na vurugu akiwa chini ya ulinzi
 Mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said
  Nyumba inayolalamikiwa ikianza kuvunjwa
 Mtaa wa Kongo ukiwa hauna mweupe
 Mtaa wa Mchikichini Kariakoo ukiwa hauna watu kutokana na vurugu zilizotokea leo
 Mtaa wa Mkunguni ambao huwa na pilikapilika nyingi ukiwa mtupu kufuatia wafanyabiashara kufunga biashara zao
Nyumba inayolalamikiwa inayogombewa na pande mbili.

1 comment:

Anonymous said...

Siamini kuona watu wanashika damu ya mtu mwingine bila gloves!