Eda Sylvester (katikati) akiwa na mshindi wa pili Flaviana Maeda (kushoto) na mshindi wa tatu Catherine Masumbigana (kulia).
MREMBO Eda Sylvester usiku huu amefanikiwa kutwaa taji la Redd's Miss Temeke 2012 katika kinyang'anyiro kilichofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam. Eda Sylvester mwenye umri wa miaka 21 anatoka katika kitongoji cha Kigamboni na ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua Shahada ya Sanaa. Eda anapendelea kusafiri na kuangalia filamu. Matarajio ya mshindi huyo ni kuwa msanii wa kimataifa na mfanyabiashara mwenye mafanikio ya juu.
(PICHA / HABARI : ERICK EVARIST, MAULID KILINDA, LUQMAN MALOTO NA CLARENCE MULISA / GPL)
1 comment:
Sisi tunamjua Miss Temeke mmoja tuu wa KUDUMU wa Washington DC.
Post a Comment