Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini hati mbele ya kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT)
----
Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeeleza kuwa Gazeti la Dira ya Mtanzania newspaper limedhalilisha taaluma ya uandishi wa habari kwa kuchapisha taarifa za kashfa dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa bila kumpa nafasi ya kujibu.
Akitangaza uamuzi wa kamati hiyo iliyoketi Jijini Dare s Salaam Septemba 20,2012, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji Thomas Mihayo alisema madai yaliyochapishwa na gazeti hilo yanaudhi, yanadhalilisha na yanaleta dharau.Vile vile taarifa ya gazeti hilo ya madai kuhusu Rais Kikwete ni ya hatari na sawa na uhaini, alisema Jaji MihayoJaji huyo pia alisema kuwa gazeti hilo pia limeivunjia heshima kamati hiyo kwa kutoa taarifa fupi tu kuwa haitawakilishwa kwenye kikao chake cha usuluhishi.
Katika kikao hicho kamati hiyo pia ilitoa uamuzi kwa malalamiko ya kampuni ya Human Capital Investment Group Limited dhidi ya gazeti la Rai toleo namba 966 la April 5, 2012.Kuhusu malalamiko ya Lowassa kamati hiyo iliamua kuyasikiliza upande mmoja baada kuarifiwa na Kaimu Katibu wa Kamati kwamba mwakilishi wa Dira ya Mtanzania hatakuwepo kwa vile mhariri wake Charles Mulinda alikuwa safari.
Malalamiko ya Lowassa yaliyowasilishwa kupitia mawakili wa kampuni ya Imma advocates, yalipokewa na MCT Novemba 11, 2011.
Waziri mkuu huyo wa zamani alikuwa analalamikia zaidi ya habari sita ambazo zilimkashifu. Habari ya kwanza ilichapishwa katika Dira ya Mtanzania toleo na 120 la Oktoba 6 – 9, 2011 iliyokuwa na kichwa cha habari Lowassa, Chenge tena” ikifuatiwa na habari mbili katika toleo na 123 la Oktoba 17-19, 2011 kwenye ukurasa wake wa kwanza zikiwa na vichwa vya habari Nape atonesha kidonda – akumbusha Mwalimu alivyomkataa Kapteni Lowassa na Kapteni Lowassa atajwa kwenye vurugu za CCM Arusha.
Katika toleo la 125 la Oktoba 24-26, 2011 ukurasa wa kwanza gazeti hilo lilichapisha habari Kapteni Lowasa, Kikwete basi.
Katika toleo la Oktoba 31- Novemba 1, 2011 ukurasa wa kwanza gazeti hilo lilichapisha habari yenye kichwa Kapteni Lowassa anaandaa mashitaka wakati katika toleo 128 la Novemba3-6, 2011 pia kwenye ukurasa wa kwanza, lilichapisha habari yenye kichwa Askofu Mokiwa amkana Kapteni Edward Lowassa.
Gazeti hilo pia lilichapisha habari kwamba CCM yapambana na Kapteni Lowassa Akiwasilisha shauri lake mbele ya Kamati hiyo ya Maadili yenye wajumbe watatu, Lowassa alisema kuwa maombi yake kadhaa ya kutaka kuweka sawa habari hizo na kuzikanusha hayakushughulikiwa.
Alipoulizwa na Jaji Mihayo kwa nini gazeti hilo lilifanya hivyo licha ya juhudi zake, Waziri mkuu huyo wa zamani alisema anafikiri lilikuwa linatumiwa ingawa sina ushahidi. Hapo alisema anaomba apendekeze kuwepo kwa sheria zitakazodhibiti vyombo vya habari ambavyo vinakashifu watu makusudi kuwaharibia.
Kuhusu madai kuwa anakosana ana Rais Kikwete, Lowassa alisema hiyo ni uhaini kutofautiana hadharani na mkuu wa nchi.
“Kama rais angekuwa mtu mwingine anayefuata habari za magazeti unatiwa ndani”, alisema. Jaji Mihayo alikubaliana naye kuhusu suala hilo la kumsema rais aliye madarakani kuwa ni uhaini.Dira ya Mtanzania iliamriwa kumuomba radhi Lowasa na kumlipa fidia zote alizoingia katika shauri hilo.
Katika shauri lingine gazeti la Rai limelalamikiwa kwa kuchapisha katika toleo lake la Aprili 25, 2012 kuwa TGNP yatapeliwa 270 mil/- Bagamoyo. Yanunua kiwanja kilichopo eneo la EPZ. Iliuziwa na kampuni ya Human Capital Investiment.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Zuhura Muro ambaye aliiwasilisha mbele ya kamati hiyo alisema kuwa taarifa ya gazeti hilo imeichafua kampuni hiyo na vile vile kumharibia sifa yeye na hata familia yake. Mhariri Mtendaji wa New Habari inayochapisha gazeti hilo la Rai Prince Bagenda alikiri kuwa gazeti hilo lilikosea na akaahidi kuchapisha taarifa ya kuomba radhi.Kamati hiyo ya MCT iliamuru kampuni hiyo kuomba radhi kwenye ukurasa wake wa kwanza..
This Day
1 comment:
habari yenyewe hajakaa fresh mtindi mkali tuu huu wacha mafisadi wachomwee
Post a Comment