ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 25, 2012

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Wafanyabiashara maarufu kama 'Machinga' wakimshawishi mteja aliyekuwa ndani ya gari kununua nguo,imekuwa ni tabia ya wachuuzi hao kuwazonga wateja wanaponunua bidhaa mbalimbali. (Picha na Anna Titus
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala ya jijini Dar es Salaam, wakisubiri huduma ya muuzaji wa mayai (kushoto), ambapo yai moja huuzwa shilingi 300 kama walivyokutwa jana, ni vema kuzingatia kanuni za afya kabla ya kutoa huduma husika ya kuuza chakula ikiwa ni pamoja na kupima afya.  (Picha na Charles Lucas)
Wachezaji wa Shule ya Sekondari Iyunga wakishambulia la timu ya Sekondari ya Wenda katika mashindano ya kutafuta timu ya mkoa yaliyofanyika viwanja vya Youth Center jijini Mbeya. Mashindano hayo yamedhaminiwa na Coca-Cola kupitia soda ya Sprite.
wapima ramani wa Kampuni ya Ujenzi ya STRABARG inayojenga miundombinu ya Mradi wa Mabasi ya Haraka jijini (DART) wakipima eneo la Magomeni Kagera, Dar es Salaam jana. Awamu ya kwanza ya mradi huo itakamilika mwezi Machi 2013. (Picha na Charles Lucas)
Mlinzi wa Bandari, Haitham Khamis (mbele) akimzuia mshambuliaji wa KMKM, Kasim Nemshi asilete madhara langoni mwake katika mechi ya Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar iliyopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Bandari ilishinda mabao 2-1. Na Mpigapicha Wetu
Mchuuzi wa vinywaji mbalimbali akitafuta wateja kwenye Kituo cha Daladala eneo la Ubungo River Side, Dar es Salaam jana. Biashara hivyo huzifanya katika mazingira magumu kutokana na kukosa vibanda hivyo kulazimika kutembea mwendo mrefu kusaka wateja. (Picha na Charles Lucas) Picha zote kwa hisani ya Majira

No comments: