Ndugu zangu,
Jana nikiwa na wanahabari wa Mbeya wanaojifunza masuala ya Online Journalism niliwatangazia pia, kuwa Mjengwablog ambayo miongoni mwa wanahabari wale ni watembeleaji wake wakubwa inaadhimisha miaka sita ya kuzaliwa kwake. Siku ya kutimiza miaka sita ya Mjengwablog ilinikuta nikiwa vijijini kule Njombe na hakukuwa na uwezekano wa kutumia mtandao. Ni tarehe 19 Septemba.
Naam, ilikuwa Jumanne, Septemba 19, 2006. Ni siku hiyo ndipo kwa mara ya kwanza niliingiza picha ya kwanza kwenye mjengwablog na kuashiria uzinduzi wa blogu. Ni picha hiyo inayoonekana. Niliipiga eneo la Kinondoni Shamba. Tangu siku ya kwanza, niliweka wazi kwenye fikra zangu, kuwa Mjengwablog iwe jukwaa litakalomtanguliza mtu wa kawaida. Iwe sauti ya ya wale ambao sauti zao hazisikiki.
Ndio, nilidhamiria, na bado ni dhamira yangu, kuwa Mjengwablog iwe ni jukwaa la fikra huru. Kuwa iwe ni mahali kwa watu kutoa mawazo yao bila kukwazwa na mitazamo tofauti ya kiitikadi. Miaka sita imepita, nafurahia, kuwa bado naongozwa na dhamira hiyo.
Chini hapa ni maoni ya kwanza kabisa kutumwa na mtembeleaji. Na anachoandika mtembeleaji huyu kutoka India kinaakisi dhamira niliyokuwa nayo.
Bwana huyu anasema; { fakir005 } at: Tue Sep 19, 06:32:00 PM EAT said... This looks like an African blog. Once the TV showed an African milk his cow. The cow had so stretched tits. I've never seen so much stretching. The african as really stretching further to twice the original length to get any drop of milk he could get. It was obvious the cow was dry because it was too long after the birth of her calf and needed to be inseminated again.The cow just stood there while the African worked the Tits. The picture does not show anycows. But the man in the picture and the house remind me of the TV scene in the gone years."
http://mjengwablog.com
No comments:
Post a Comment