Unakumbuka ile kolabo ya P Square na Akon inaitwa Chop my money ambayo ilimfanya May D kuwa staa zaidi baada ya kuongezwa kuwa mtu wa nne kusikika kwenye hiyo single?
kama hufahamu May D ni msanii
wa Nigeria ambae alisainiwa kuwa chini ya lebo inayomilikiwa na P Square
(Square Records) ambapo ni siku kadhaa zimepita toka lebo hiyo itangaze
kwamba haimuhitaji tena na wala hayuko tena chini yao.
Leo mtandao wa Naijag umeripoti
kwamba May D ambae alitimuliwa na lebo hiyo wiki kadhaa zilizopita yuko
kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na wanasheria wake ili awashitaki P
Square kwa kuvunja mkataba kiholela.
May D anasema taarifa za
kutimuliwa kwake alizipata kwenye blogs na magazeti kama walivyopata
watu wengine na kwamba hakupewa taarifa zozote za kiofisi kama
inavyopaswa, hiyo ndio sababu inayomfanya awashitaki P Square akiwemo
kaka yao mkubwa Jude Okoye ambae ndio alitangaza kuuvunja mkataba wa May
D.
1 comment:
ndo mastar wa kinegeria walivyo sasa wabongo wagizeni style zao okay ha ha ha
Post a Comment