Chama cha Mapinduzi Zanzibar, kimesema ikiwa itatokea kuvunjika kwa Muungano wa Serikali mbili kutokana na shinikizo la baadhi ya wanasiasa ‘mapepe’ kutaibuka vuguvugu la kujitenga kwa visiwa vya Unguja na Pemba .
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alitoa matamshi hayo katika mahojiano na NIPASHE yaliofanyika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.
Vuai alisema tukio lolote litakalotoa mwanya wa kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar linaweza pia kusababisha visiwa vya Pemba na Unguja kujigawa na kuwa mbalimbali.
Alisema hakuna mwanasiasa au kiongozi wa aina yeyote atakayemudu kulizuia wimbi hilo lisitokee huku akieleza kuwa nje ya Muungano anaamini visiwa vya Pemba na Unguja ‘ima faima’ havitabaki pamoja kama ilivyo sasa.
“Wanaoshabikia Muungano uvunjike wasome alama za nyakati,Muungano ikiwa utavunjika leo, kesho au kesho kutwa, Pemba na Unguja si hasha kila upande ukabaki kwake,” alisema.
Alisema anaamini wapo wanasiasa wanaotumia mwamvuli wa ukabila na ubaguzi ili kuficha madhambi yao kwa kuamua kuwagawa watanzania bara na wazanzibari kwa lengo la kuatamia maslahi yao bila kujali uzito wa umoja wa kitaifa.
Akikumbusha matamshi ya baadhi ya viongozi yaliowahi kutolewa kuanzia mwaka 1995 na baadae mwaka 2005, alisema tayari wanachama wa CUF waliojiita wazee kutoka Pemba wakiongozwa na Hamadi Ali Mussa na Ali Makame waliwasilisha ombi maalum UN la kutaka Pemba ijitenge.
“Serikali za CCM zinatambua ubaya na madhara ya jamii kujitenga hivyo jambo hilo lilipuuzwa kwa kukosa mashiko ila naamini nje ya Muungano, Pemba na Unguja ni vigumu kubaki salama,” alisema.
Alisema wanaotaka kuvunja Muungano wamebeba ajenda tete ya kutetea ulwa na maslahi binafsi kwa kisiingizio cha kuwepo kwa kero za Muungano ambazo alidai CCM inaamini zinarekebishika na kuzungumzika.
Akizungumzia matamshi yaliotolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhusu uchaguzi wa Bububu kuvurugwa na baadhi ya wanasiasa toka CCM, Vuai alisema hakutarajia kusikia maelezo hayo yakitoka kwenye kinywa cha kiongozi huyo.
Vuai aliwatupia lawama viongozi wa CUF ambao waliojibebesha kazi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uchaguzi huo huku akidai makundi ya wanachama wao waliwazuia wananchi wasijitokeze kutumia haki ya kupiga kura kutokana na kukithiri vitisho.
Alisema vitendo vilivyofanywa na viongozi wa CUF katika uchaguzi wa jimbo la Bububu Septemba 16 i havikuwa vya kiungwana na kueleza vilikwenda kinyume na misingi ya demokrasia pia maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa.
Hata hivyo akihutubia wanachama wa CUF katika uwanja Kijichi kwa Geji mwishoni mwa wiki Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, alisema vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi wa Bububu zilisababishwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya SMZ na kumtaka Rais wa Zanzibar kuchukua hatua dhidi ya watu waliohusika.
Maalim Seif ambaye pia Makamu wa kwanza wa Rais, alisema hatakubali kuona Zanzibar ikirejea katika machafuko na kutaka SMZ iwashughulikie watu wote wanaotaka kurudisha machafuko ya kisiasa visiwani humo.
Kuhusu Muungano, Maalim Seif alisema kwa mtazamo wake mfumo wa muungano wa mkataba ndiyo unafaa kuzingatiwa wakati huu wa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania.
Hata hivyo waasisi wa Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Visiwani wameibuka na kupinga hoja ya muungano wa mkataba kwa madai ina ajenda ya siri ya kuvunja Muungano wa Tanzania.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Huyu Vuai ana wazimu nae, maana kile cheo alopewa Chimwaga anaona watu wote sasa wapumbavu. Aliemwambia nani PACHA wakatenganishwa kwa fitna, ghilba, na vitisho. Mzembe mkubwa huyu, Mungu amshinde, hasidiya allahu wahasidi rasul, mbaguzi wahed. Muungano na uvunjike na Zanzibar (Unguja na Pemba) ataziwacha vilevile.
Post a Comment