Wameandamana kutoka maeneo mbalimbali ya Dar na sasa wanafanya mkutano mkubwa viwanja vya kidongo chekundu
Na blogger team Tz
JUMUIYA na Taasisi za Kiislm nchini mapema leo wametoa tamko kali dhidi ya watu na mataifa yanayokashifu na kuhudharirisha uislam duniani kuachana mara moja kabla ya hatua kali haijafuatwa.
Wakitoa mada na dua mbalimbali leo kwenye viwanja vya kidongop chekundu, umati mkubwa na wa aina yake wake kwa waume wa kiislam waliokusanyika kutoka pembe zote za jiji la Dar es Salaam mara baada ya sara ya Ijumaa.
Akitoa tamko hilo kwa nguvu kubwa, na kuhitikiwa na umati huo Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda aliitaka Serikali kuchukua hatua za haraka ikiwemo kutoa tamko kwa hatua ya kukashifiwa kwa Uislam baada ya raia wa Marekani kutengeneza filamu ya udharirishaji.
Shehe Ponda aliitaka Serikali ya Tanzania kuzuia mitandao ya intaneti , dvd na mianya mingine kuacha mara moja kuendelea kuonyesha filamu hiyo ya kumkashifu mtume, huku wakitaka ubalozi wa Tanzania ufungwe mara moja.
“Tamko hili ni la waislam wote wanaompigania Mtume, kuanzia sasa waislam tunagomea bidhaa zote zinazotengenezwa na Marekani pamoja na nchi ya Izraeli na Ubalozi wao hapa nchini ufungwe la sivyo tutachukua hatua zaidi” alisema Sheeh Ponda.
Pia alisema kuwa, suala la kuondolewa kwa Mufti wa Tanzania, Shaaban Simba lipo palepale ambapo wapo katika mipango mikubwa ya kufanya mageuzi ilikuondoa ukandamizwazji wa Uislam dhidi ya watu wachache wanaotumia mwanya iliopo Baraza la waislam Bakwata.
“Kuondoa uongozi wa Bakwata na ule wa Baraza la Mitihani Necta upo palepale, tunafanya mipango mikubwa na tutapiga ndege wanne kwa jiwe moja” alisema Ponda huku akishangiliwa na waislam wote waliokusanyika viwanjani hapo
Hata hivyo awali waislam hao nusura zitokee vurugu kubwa baada ya jeshi la Polisi kuuzingira uwanja huo na kuweka alama za hatari ili waislam hao wasikusanyike ndani ya viwanja hivyo, lakini kwa umoja wa waislam hao walijitoa muhanga na kukaidi amri iliyowekwa na askari wa FFU ambapo walikata uzio huo na kuingia kwa wingi.
Waislam hao ambapo waliwatanguliza wanawake, wakiingia hapo huku wakitaja jina la mtume sambamba na mabango yao, waliweza kuwazidi maharifa Polisi na kufanikiwa kuingia ndani huku makundi mengine muda huo huo nayo yakapata upenyo wa kuingia ndani humo.
Kwa hali hiyo jeshi hilo lililazimika kuwaachia licha ya awali kuvunja vifaa vya saiti na kuvizuia kwa muda hasa baada ya kuona umati mkubwa ukiendelea kukusanyika, iliwarudishia na baadae kuweka ulinzi mkali huku wakiwa na magari zaidi ya 10.
3 comments:
wanaelewa alietengeneza movie ni muEgypt na sio mmarekani? haya mambo ya kuandamana bila kujua kiini sio mazuri wananchi
wanaelewa sana ndugu yangu aliye tengeneza movie ni mu egypt na ilipotengenezwa walikuwa hawajamkusudia mtume wetu lakini kwa propaganda zao kutaka kuanzisha vita na iran ndo wakamuweka usifanye watu mbu mbu bu wewe, na huyo mu egypt si ndo ametumwa na hao hao wamarekani na wa israel,watu hawako hamsini kweusi bwana mdogo,waislamu popote pale wapo tayari ulimwenguni kote wamesha vaa nguo wanasubiri lipstik watoke uwanjani.
usisikiye bwana mdogo watu wanachunguza mambo na siyo kikuru kakara kurukia mambo so pao moto usileta za kitoto kula baga hapo kwa bro dj luke sisi wacha tunywa maji ya kisimani na bongo yetu lakini kutukaniwa kwa mtume wetu hatukubali tutamwaga damu
na nawaunga mkono waislamu wote wa tanzania kwa kuandamana na kuamka dini yenu ni bora na lazima muupiganiye siyo kupigania vyama vya siasa
mdau from kariakoo gerezani mtaa walindi
alhamdulillahi rabii laalamin mungu akujaliyehi kila la kheri na mshikamane hivi hivi daima waislamu wote wa tanzania na popote pale walipo siiyo kukaa na kugombania siasa na huku dini na mtume wenu anakashifiwa, nimefurahi sana kuona picha hii na ummoja wenu
Post a Comment