ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 12, 2012

KUNGUNI WA MTONI KICHANGANI

 mmoja wa wakazi hao BIBI KOKU, akieleza namna alivyo athiriwa na kunguni hao.

Kunguni wamekuwa tishio kwa wakazi wa kitongoji cha mtoni kichangani manispaa ya temeke jijini dar es salaam. Ambapo wadudu hao wamewafanya wakazi hao kukosa usingizi kabisa, hali kadhalika ngozi za miili yao zimeathiriwa.

Tatizo hilo lapata mwaka mzima sasa kila wakimwagia Dawa bado hali inazidi kuwa tete, licha ya Waziri wa wizara ya AFYA NA USITAWI WA JAMII. Dr. hussein mwinyi, kukiri kuwa serikali inacho kitengo cha kukabiliana na Wadudu kama hao bado msaada kwa wakazi hao haupatikani.
Juhudi za kampuni ya SUMMIT SERVICES ya Sinza kuangamiza wadudu hao inaonekana kugonga mwamba kila wakipulizia dawa kunguni hao wanaongezeka.
 Dawa ya kuulia kunguni inachanganywa
 
mkurugenzi wa kampuni SUMMIT SERVICES akiwa tayari kuanza kazi
kitanda kikimwagiwa dawa ya kuwaua kunguni hao..

Habari zaidi usikose kusikiliza kipindi cha weekend spacial''FROM KITONGOJI'' Wapo radio fm 98.00mhz jumamos th.13 OCT 2012 saa nane mchana.

1 comment:

Anonymous said...

Inawezekana ikawa hizo dawa za kuulia kukunguni ni katika madawa "feki" ndio maana hazifanyi kazi