ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 10, 2012

Wauza nyama za wizi wasakwa


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema jeshi la Polisi kisiwani Pemba limeanzisha msako mkali wa kuzitafuta bucha zinazouza nyama ya wizi ikiwa ni hatua ya kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likizidi kila kukicha.

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kufuatilia suali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF), Saleh Nassor Juma, aliyetaka kujua ni kesi ngapi hadi sasa zilizofikishwa polisi.

Mwakilishi huyo pia laitaka kujua iwapo kuna kesi ambazo zimeshapelekwa mahakamani, na kama kuna bucha zozote zilizotuhumiwa kwa wizi huo na kama kuna wamiliki wa bucha hizo wameshawahi kuhojiwa na jeshi la polisi.

Waziri Aboud, wakati akijibu suali hilo alisema ni kweli kumekuwa na kesi zilizofikishwa katika vituo vya polisi zinazotokana na wizi wa nyama na tayari jeshi la polisi limeanzisha utaratibu wa kuzifuatilia na watakaobainika kufanya hivyo watafikishwa katika mkono wa sheria.

Alisema katika kulifanyia kazi suala hilo tayari hivi sasa kuna malalamiko manne yanayohusu wizi wa mifugo ambayo yamefikishwa Mahakamani huku akiwashauri wananchi kutoa taarifa za kihalifu iwapo wana mashaka na watu wa aina hiyo.

Aboud alisema malalamiko hayo yaliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Chake Chake Pemba kuanzia Januari hadi mwezi Septemba 2012, ambapo matatu tayari yametolewa hukumu na kesi moja inaendelea kusikilizwa Mahakamani.


Aidha aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba katika kukabiliana ana tatizo hilo Jeshi la Polisi tayari ilibaini kuwapo kwa tuhuma za bucha iliyopo Macho manne kutumiwa na wezi wa ng’ombe ambapo mmiliki wake aliitwa Polisi kuonywa vikali.

Waziri huyo alisema baada ya kujitokezaa hilo tayari hali hiyo imeonekana kuaza kupata mafanikio kutokana na kutokuwapo kwa malalamiko ya aina yoyote yaliyowasilishwa Polisi hadi sasa.

Hata hivyo Waziri huyo aliseama chanagamoto kubwa ambayo inajitokezaa katika kushughulikia kesi za aina hiyo baadhi ya wanajamii kuamua kuingilia kesi za watuhumiwa waanaoshutumiwa kufanya vitendo vya aina hiyo kwa kuwapa misamaha.

Alisema hali hiyo imejitokezaa kwa kuwapo mifano halisi ya matukio ya aina hiyo ambapo kati ya kesi hizo zilizoripotiwa zimeweza kumalizika kwa njia ya kufahamiana kifamilia ikiwemo kesi iliyotokea katika eneo la Chake Chake.

Kuhusu madai ya sheria iliopo huenda kuwa haiana nguvu Waziri huyo alisema sio kweli kwani sheria iliopo ina mapungufu ila kumekuwa na tatizo la wananachi kuoneana imani baada ya kuonekana kesi zinazofikishwa mahakamani kuwa na ushahidi kamili jambo ambalo huamua kuziondoa mahakamani.

Mwakailishi wa Wanawake Mwaanajuma mdachi aliulizaa ni kwanini wananchi anaopatikana na makosa ya aina ahiyo wamekuwa wakichukuliwa hatua mikononi mwa wananchi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Akijibu hilo Waziri Aboud, alisema ni kweli kumekuwa na hali kama hizo zinazojitokeza akatika jamii baada ya watu kuamua kufanya vitendo vya aina hiyo lakini wanaofanya vitendo hivyo bado wanaenda kinyume na sheria kwani hairuhusu mtu kujichukulia sheria mikononi.

Hata hivyo Waziri huyo alisema bado Polisi ina uwezo mkubwa wa kushughulikia kesi za wizi wa mifugo ili kukomesha tatizo hilo ili kuwafanya wananachi waendelee kufanya shughuli hizo kupata maendeleo yao.

No comments: