ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 13, 2012

Wichita chupuchupu kwa Houston watoka 1-1

Timu ya soka ya Jumuiya ya Watanzania kutoka Wichita, Kansas leo jioni walipambana na wenzao wa jiji la Houston, Texas katika mchezo wa kukata na shoka uliochezwa kwenye viwanja vya Fondren.
Kikosi cha Houston

Kikosi cha Wichita
Matokeo ya mechi hiyo yalikuwa ni 1-1 .Katika mchezo huo uliochezeshwa vyema na refarii wa FIFA Javier Hernadez wenyeji ambao kama wangekuwa makini wangetoka na ushindi mnono ndiyo waliotangulia kupata bao katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza kwa bao safi lililofungwa na striker Ally Mtumwa aka Giroud baada ya kumalizia gonga kama 8 hivi za wachezaji wa Houston. 
Wichita walipata bao la kusawazisha dakika ya 38 kipindi hicho cha pili kupitia kwa striker wao Iddy Ligongo aka Bicco ambaye aliyatumia vizuri makosa ya golikipa John Kijani wa wenyeji aliyeshindwa kuokoa mpira ambao ulipigwa na Deo Ngassa na kuonekana hauna madhara yoyote.
Kipindi cha pili wenyeji walikuja juu na kama si uhodari wa golikipa wao Abuusaady Saadiq basi matokeo yangekuwa tofauti.Mashuti mawil yaliyopigwa na winga teleza Sekulu na Stiker Bitebo yaligonga miamba na refarii Hernandez alipeta penati dakika za lala salama.
WICHITA wanategemea kuanza safari ya kurudi Kansas jumapili asubuhi wakati Houston wana mechi ya kugombea kombe la Afrika jumapili hiyo jioni katika viwanja vya Kellough High School
Wichita wakiingia uwanjani



Houston wakijadiliana kabla ya mechi

Mkakati wa mechi.Team Houston

Mwalimu Juma

Shabiki No.1 wa Wichita

Raheem Chomba

Mtanange ukiendelea

Mtanange ukiendelea

Mashabiki jukwaa kuu

Jimmy Makwega Zenden na Iddy Ligongo

Mashabiki

No comments: