TIMU ya Ashanti United jana iliivurumisha bila huruma Moro United mabao 10-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulionekana dhahiri kuwa wa upande mmoja kutokana na wachezaji mahiri wa Moro United kutokuwepo, Ashanti walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza mabao 5-1.
Moro ambayo mlinda mlango wake alikuwa bonge la mtu alikuwa akijigararagaza kila wakati kwa madai akaumia.
Mabao ya Ashanti yalifungwa na Lambele Jerome alifunga mabao sita dakika ya 35, 52, 71, 76, 81 na 89, Shabani Hatibu alifunga matatu dakika ya nane, 11 na 37, na Raju Mahmoud dakika ya 16.
Bao la Moro United lilifungwa kwa njia ya penalti na Twahir Kiparamoto dakika ya 21.
Kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani Green Warriors na Polisi Dar es Salaam zilitoka sare ya kufungana bao 2-2.
Mabao ya Green Worriors yalifungwa na Said Asaa dakika ya 80 Edward Kheri dakika ya 89. ZAID TEMBELEA http://pallangyor.blogspot.
No comments:
Post a Comment