ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 26, 2012

Baba Mdogo wa Mwigizaji wa Filamu Marehemu John Maganga Aeleza Mkasa Mzima toka Alipo anza kuumwa Mpaka kifo chake


Marehemu John Stephano Maganga, wakati wa uhai wake.

Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya, ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.

Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, ameelezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.
Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha anaendelea na kusema siku ya pili yake John alimpigia simu na kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii vizuri, kuona hivyo, baba yake mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta amelala kwenye kochi anatoka jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?, John akamjibu, tumbo linamuuma sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake mzazi nimwambie tumpeleke Hospital Mwananyamala.
Tulipofika pale hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari wakaamua wampige X Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu makali sana tumboni mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari, wakasema ana matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji wa haraka.
Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura (emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.
Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi nilifika Muhimbili na kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku wa jana yake. Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha kinachoendelea. Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu yule daktari ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani anamshughulikia hivyo alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza punguza makali ya sumu iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip ya maji lakini inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.
Muda mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena, amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake. Mazishi yamepangwa kufanyika makaburi ya kinondoni kesho. Alisema baba mdogo wa muigizaji Stephano.
Habari kwa hisani ya Bongo 5

4 comments:

Anonymous said...

THIS IS A LAW SUIT!!!! ARE THESE DOCTORS TAKE KIAPO AT ALL WAKIMALIZA DEGREE HIZI ZA UDAKTARI KAMA HUKU STATES???? YAANI HUYO DOCTOR NI MMOJA TUU NA HANA MOBILE PHONE??? JAMANI HIZI HADITHI NDIYO ZINATUFANYA TUNG'ANG'ANIE HUKU MAJUU! UWE MLALA HOI UWE TAJIRI UKIUGUA UTAONA JINSI MADAKTARI WANAVYOKIMBIA KUSERVE YOUR LIFE! WANAPIGIANA SIMU NA KUPEANA USHAURI, THIS IS A LOSS OF HUMAN LIFE JAMANI SOMEBODY'S SON, BROTHER, FATHER OR FATHER TO BE, FRIEND AND AT MOST BINAADAMU! YAANI MADAKTARI WANAONA MTU ANA ORGAN ISSUE MNAMWACHA ANALALA HUKU KONGOSHO (PANCREASE) INA MATATIZO? BIOLOGY GANI HIYO WALIYOSOMA?? Mimi si daktari but nimesoma science enough to know that unaweza kuishi bila hii kitu. The pancreas has two main functions: secretion of insulin, which controls blood sugar levels, and secretion of digestive enzymes and hormones. You can live without it it does not function well, although this is not a perfect solution, these functions can be replaced through insulin injections and oral pancreatic enzymes with meals!!!!!!! Wangeiondoa the same day huyu kijana jamani angepona tuu. OMG WHAT A LOSS. Serikali inabidi iangalie kuinvest in educating doctors wenye speciality ambazo ni rare in Tanzania or improve out MD schools ili hawa madaktari wawe na uhakika na diagnosis than making a guess work. The blood chemistry of this guy would have a lot of flags (out of range) on sugar level, and other things right there you should know its an ORGAN ISSUE WHETHER IS LIVER OR PANCREASE THEN YOU DO THE ORGAN FUNCTION TESTS (IF THEY EXISTS) THEN YOU RULE OUT WHICH ONES, MBONA HUKU KUNA GUIDELINES HATA UKIGOOGLE ITAKUAMBIA NINI CHA KUANGALIA UKITAKA KUJUA LIVER AU FIGO AU KONGOSHO ZINAFANYA KAZI, I REALLY CRIED READING THIS STORY ITS SO SAAAAAAAAAAAAAAAAAD. BONGO SIRUDI. NINTAZEEKEA HUKU HUKU I KNOW I DO NOT HAVE TO KNOW NOBODY TO GET 1ST CLASS HEALTH CARE AS FAR AS U HAVE MEDICAL INSURANCE, ASANTE OBAMA FOR OBAMACARE.

Anonymous said...

mdau calm down i feel you too, na mimi kwa kweli nimekasirika mchanganyiko wa hasira na huzuni vyote vimenitawala hapa mtu anasema utumbo umekatika whaaat? tunaenda wapi Tanzania hao madaktari wamesoma au ndio vyeti vya kununua mradi siku ipite god, wabongo sijui tuanzie wapi tupate ufumbuzi mean while tupeane pole inauuma kusikia kisa hiki

Anonymous said...

mdau hapo juu .... ulipotokea mgomo wa madaktari wewe ulikuwa wapi?.... ndiyo baadhi ya mambo yaliyozungumziwa, serikali ikaweka propaganda na siasa na kugeuza madai yote ya madaktari .... mwishoni kwa dharau wanaambiwa wasiotaka kazi waache waende kokote wanakotaka .... matokeo hao wataalam wachache tulionao wameondoka, kama wamebaki nchini wengi wako hospitali binafsi .... na hata huyo mmoja ambaye hakua zamu si ajabu angepigiwa simu asingepokea maana anaweza kuwa alikua kwenye hospitali binafsi anatibu wagonjwa wa aina hiyo hiyo kujiongezea kipato cha kutunza familia yake katika muda wake ambao sio wa kazi ... watanzania waamke sasa na kudai haki zao serikalini sio kulalamikia madaktari ambao wanaenda kukesha hospitalini on call kwa shilingi 10,000 - 25,000 kwa siku wakati hiyo ni change tu salio la simu kwa watu wengine serikalini wanaoishi kwa hela za vikao vya nusu saa na wanapata si chini ya shilingi 60,000

Anonymous said...

I happen to have knowledge of medicine, from what it sounds he may have suffered from a condition called acute necrotizing pancreatitis if that is the case the mortality is very high either way. Pancreatic surgery requires expertise not commonly available especially in Tz and even at the hands of a pancreas surgeon mortality remains high since many things can go wrong. Also with knowledge of healthcare in Tz for the longest time other than at Muhimbili most hospitals did not run labs onsite but sent them to the central lab at Muhimbili. I don't know if Mwananyamala hospital now runs it's own labs I.e. Chemistry panels? Having said that, you just need to be lucky with any sickness in Tz. In most health facilities the providers are doing the best they can under the circumstances (which of course is not good enough in the west) and I am assuming his pancreatitis which can mimic an acute abdomen is the reason they wanted to perform surgery in the first place.