Kolonia Santita ni shirika la madawa ya kulevya au 'drug cartel'. Panthera Tigrisi ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya ambaye ni katili kuliko wote katika Latino na Hemisifia ya Magharibi. Kitabu hiki kinahusu ujasusi, madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania.
Kitabu hiki kimetungwa na mtunzi anayekuja juu akiwa ni mjomba kabisa wa mtunzi maarufu wa riwaya za kijasusi Marehemu Elvis Musiba ambaye alitamba na kitabu chake cha kwanza cha 'Njama'.
Enock Maregesi ambaye anaishi na kufanya shughuli zake kwa Malkia Elizabeth anasema kitabu hiki amekifanyia kazi kwa umakini na kitaleta mapinduzi kwenye uandishi wa Riwaya za Kiswahili za Kijasusi.
“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.” - www.goodreads.com
Kwa habari zaidi wasiliana na Enock Maregesi kupitia ukurasa wake wa Facebook: http://www.facebook.com/pages/Kolonia-Santita/462971887081149 au kupitia blogu ya enockmaregesi.wordpress.com. Kwa wapenzi wa vitabu kaeni mkao wa kula kwani kiko njiani na kitapatikana kwenye bookstores zote Afrika Mashariki. Kinapatikana pia Amazon, Authorhouse na maduka mengine yote makubwa ya vitabu ya mtandaoni
No comments:
Post a Comment