Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik akimkaribisha Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada ya kuwasili kutokea Kampala, Uganda ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabilamjini Kampala Uganda leo baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa makuu. Mkutano huo ulijadili hali ya usalama ya Mashariki ya DRC eneo ambalo limetekwa na waasi wa kikundi cha M23. Baadae Rais Kikwete na ujumbe wake walirejea jijini Dar es Salaam.
(Picha na Freddy MARO-IKULU)
No comments:
Post a Comment