ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 26, 2012

SPIKA ANNE MAKINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA MZEE RAJANI, UPANGA JIJINI DAR


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili nyumbani kwa marehemu mzee Shree Jayantilal Pragji Rajani, maarufu kama Mzee Rajani kuhani Msiba. Mzee Rajani alifariki Jumatano Novemba 21, 2012 mjini London alikokuwa amelazwa.

Spika Anne Makinda akisaini kitabu cha waombolezaji.

Mzee Pius Msekwa na Anne Abdallah wakisaini kitabu cha waombolezaji.
Kwa picha zaidi bofya read more
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza waombolezaji kuweka maua katika mwili wa Mzee Rajani ikiwa ni ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa marehemu wakati wa kuaga mwili wa marehemu MzeeRajani nyumbani kwake Upanga.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula wakitoa heshima 
zao za mwisho kwa mwili wa mzee Rajani.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mzee Salim Ahmed Salim.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mmoja wa Waombolezaji, katikati ni Rostam Azizi.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mzee Kingunge.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Akisalimiana na Mama Anna Mkapa.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mzee Pius Msekwa.(Picha zote na Owen Mwandumbya, Bunge)

No comments: