Wakazi Goziba watakiwa kutumia huduma Mtandao wa Vodacom kuimarisha usalama
* Vodacom yawa ya kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika kisiwa hicho
* Wakazi wake waweweseka kwa furaha. Wamuhakikishia RC kuulinda mnara kwa nguvu zote
* Wasimamisha shughuli kisiwani kushuhudia uzinduzi
* Wakazi wake waweweseka kwa furaha. Wamuhakikishia RC kuulinda mnara kwa nguvu zote
* Wasimamisha shughuli kisiwani kushuhudia uzinduzi
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali (Mst), Fabian Massawe akiuzindua rasmi mnara wa mtandao wa Vodacom katika kisiwa cha Goziba tayari kutoa huduma kwa wakazi wa kisiwa hicho. Kushoto kwake ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo. Vodacom imekuwa mtandao wa kwanza kufikisha huduma za simu za mkononi katika kisiwa hicho cha ziwa Viktoria ikiwa ni utekelezaji wa azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote katika mtandao wa huduma za simu za mkononi na kuwawezesha kubadili maisha yao.
Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea na wakazi wa kisiwa cha Goziba wakati wa halfa ya uzinduzi wa huduma za Vodacom kisiwani humo ambapo ni mara ya kwanza kwa kisiwa hicho kupata huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. Salum aliwahimiza wakazi hao ambao wengi wao wafanyabiashara ya samki kutumia huduma ya M-pesa kujihakikishia usalama wa fedha dhidi ya matukio ya uporaji na uvamizi ziwani na katika ksiwa hicho kwa ujumlaSehemu ya umati wakazi wa kisiwa cha Goziba wakiitikia salama ya maendeleo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali (mst)Fabian Massawe wakati w ahala ya uzinduzi rasmi wa huduma za Vodacom katika kisiwa hicho. Vodacom imekuwa kampuni ya kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu z amkononi katika kisiwa hicho cha Goziba kilichopo katika ziwa Viktoria.
Baadhi ya wakazi wa kisiwa cha Goziba wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe (nyuma mwenye kofia nyekundu) mbele ya mnara wa Vodacom mara baada ya uzinduzi rasmi wa huduma za Vodacom kisiwani hapo ambazo ni huduma za kwanza za mawasiliano ya simu za mkononi katika historia ya kisiwa hicho kilichopo katika ziwa Vikroria, wilaya ya Muleba.Kushoto kwa RC Massawe ni Meneja Mahusino ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo na Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage
Kutoka Kushoto Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali(Mst) Fabian Massawe, Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Salum Mwalim na Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera Avera Mosha wakifurahia kuanza rasmi kwa huduma za Vodacom katika kisiwa cha Goziba. Vodacom imekuwa kampuni ya kwanza ya simu za mkononi kufikisha huduma katika kisiwa hicho cha Ziwa Viktoria ikitekeleza azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote katika mtandao wa huduma za simu za mkononi na kuwawezesha kubadili maisha.
Wakazi wa kisiwa cha Goziba kilichopo wilayani Muleba mkoani Kagera wamepokea kwa mara ya kwanza huduma za simu za mkononi katika historia ya kisiwa hicho kufuatia kampuni ya Vodacom kuzindua huduma zake kiswani humo.
Akizindua rasmi huduma hizo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe amewataka wananchi kutumia uwepo wa huduma za mawasiliano kukabiliana na changamoto za kiusalama kwavkutoa taarifa za uhalifu ama viashiria vya uhalifu kwa vyombo husika mara tu wanapoona dalili.
"Kuwasiliana ni kitendo cha maendeleo na sasa Goziba imeunganishwa na ulimwengu mzima na wakati tunapoishukuru Vodacom kwa kutuletea huduma hii nasi lazima tujipange kuitumia tunu hii kuleta tija zaidi katika maisha yetu na shughuli za kiuchumi tunazojishughulisha nazo."Alisema Massawe.
Kanali Mstaafu Massawe amesema kwa miaka mingi kisiwa cha Goziba kimekuwa katika usalama kufuatia vitendo vya uporajia na uvamizi majini na hivyo wavuvi na wakazi koiujikuta wakipoteza mailioni ya mali ikiwemo maboti, mashine za uvuvi na nyavu.
"Hatuna budi kusema uhalifu sasa basi tutumie uwepo wa huduma za mawasiliano kupitia mtandao wa Vodacom kuimarisha ulinzi ziwani kwa kupeana tahadhari tunapohisi dalili za ujambazi pamoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili kuchukua hatua mara moja, hapo kabla haya yote hayakuwezekana kwa sababu hatukuwa na huduma za mawasiliano na hivyo kwa kiasi fulani kutoa mwanya kwa wahalifu". Alisema Mkuu huyo wa Mkoa Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Bw Salum Mwalim alisema Vodacom kufikisha huduma za mawasiliano ya simu za mkononi katika kisiwa cha Goziba ambacho ni maarufu kwa shughuli za uvuvi katika ziwa Viktoria ni utekelezaji wa mpango mkakati iliyouahidi kwa umma wa kwamba itaendelea kuwekeza katika maeneo yasiyo na huduma za mawasiliano pamoja na kuboresha mawasiliano katika maeno ambayo tayari mtandao wa Vodacom unapatikana.
"Ni siku ya furaha kwetu sote kuona Vodacom ikiendelea kupata mafanikio katika azma yake ya kuwaunganisha watanzania kimawasiliano ili kuwawezesha kutumia teknolojia za simu za mkononi kuboresha maisha. Leo Vodacom imebadili historia ya kisiwa cha Goziba kwa kukipatia huduma za mawasiliano ya simu za mkononi."Alisema Bw. Mwalim "Tambueni fursa za kiteknolojia zinazopatikana katika Vodacom ikiwemo huduma ya M-pesa itumieni huduma hii kwa kuachana na tabia ya kusafiri na fedha ziwani na hata kukaa anzo katika makazi yetu na hatimae kutoa ushawasishi kwa majambazi, katika kisiwa hiki hakuna benki ila kupitia M-pesa sasa mnayo huduma salama, rahisi na ya uhakika ya kibenki." Aliongeza Bw Mwalim Kampuni ya Vodacom imepanaga kutumia zaidi ya 200 Bilioni katika mwaka wa fedha unaoishia Machi 2013 kupanua mtandao wa huduma zake na kuboresha ubora wa huduma katika sehemu mbalimbali nchini.
Baadhi ya wananchi walisikika wakisema kwamba sasa Goziba imekamilika huku wakimuahidi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Massawe kuulinda mnara huo na miundimbinu yake kama heshima kwa kampuni ya Vodacom kwa kuwakumbuka na kuwajali.
Shughuli katika kisiwa hicho zilisimama kwa mamia ya wananchi kuhudhuria hafla ya uzinduzi iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lemris Kipuyo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ACP Philip Kalangi.
No comments:
Post a Comment