Thursday, December 6, 2012

KUVAA KHANGA MOJA KUNAVYOWEZA KUISTAWISHA/KUISAMBARATISHA NDOA YAKO!

UHALI gani mpenzi msomaji wangu? Maandalizi ya Krismasi na Mwaka mpya yanakwendaje? Ni matumaini yangu kila kitu kinakwenda sawa, kikubwa nikukumbushe tu kumuomba Mungu atujaalie kuuona mwaka wa 2013 tukiwa wazima.
Ndugu zangu, katika ulimwengu wa sasa, walio kwenye uhusiano wanatakiwa kuwa makini sana kuhakikisha kwamba wanadumu.
Vishawishi vimekuwa ni vingi kwa wapenzi na hata kwa wanandoa kiasi kwamba kila siku tumekuwa tukisikia ndoa ya fulani imevunjika, mara fulani na fulani wamemwagana kisa wamesalitiana.
Katika hili leo nataka kuzungumzia tabia ya baadhi ya wake za watu kujitafutia usumbufu kwa wanaume wakware kwa kuwavalia mavazi ya kimitego.
Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, mtu hachaguliwi nguo ya kuvaa bali yeye mwenyewe anatakiwa kuangalia anavaa nini wakati anakwenda wapi au yuko wapi. Nilisema hivyo kwa kuwa nimeona mavazi hayo yamekuwa yakichangia usaliti na hatimaye uhusiano wa wengi kuingia kwenye migogoro.
Unakuta msichana amefungashia ile mbaya lakini anakatiza mbele za wanaume marijali akiwa amevaa ‘kitaiti’ kinachoonyesha hadi ‘mazagazaga’ yake kiunoni. Ukifuatilia zaidi unakuta ni mpenzi wa mtu, sasa hapo jiulize anachotafuta msichana huyo ni kipi?
Achilia mbali hao ambao hawajaolewa kwani naweza kusema kuwa wanakuwa micharuko kutokana na kukosa wanaume wa kuwatuliza, kuna hawa wake za watu ambao nao wanaingia huku.
Kuvaa khanga moja kwa mwanamke huku ndani akiwa hajavaa chochote ni mtihani mkubwa kwa mwanaume. Kitendo cha mke wa mtu tena anayeishi kwenye nyumba ya kupanga kuvaa vazi hili kisha kukatiza kwenye korido akitokea au kwenda kuoga hatari sana.
Mbaya zaidi mwanamke huyo anavaa khanga nyepesi halafu anatembea kwa staili ya ‘hamsini…mia….hamsini…mia’, yaani kwa makusudi analitingisha wowowo lake ili kuwadatisha wale wanaomuangalia, huu si ulimbukeni jamani?
Ifike mahali tuzionee huruma ndoa zetu, tuziheshimu na tuziwekee mbolea ili ziweze kudumu. Tusiwe sababu ya kuachika kwetu kwani wapo wanaozitamani ndoa lakini hawapati wa kuwaoa.
Niseme tu kwamba vazi la khanga moja si sahihi kuvaliwa mbele za watu, hili lina sehemu yake maalum ambako ukilivaa unaweza kuinogesha ndoa yako. Ndiyo maana kuna wanaosema khanga moja kamvalie mumeo chumbani, hawa wako sahihi kabisa.
Kama utakuwa ukilitumia vazi la khanga moja unapokuwa chumbani na mumeo au mnapokuwa mnaishi kwenye nyumba yenu na hamna watoto, unaweza kuistawisha ndoa yako.
Kivipi? Kwanza anapokuwa ndiyo karudi kazini hata kama atakuwa amechoka vipi, lazima atahitaji ‘mambo yetu’. Hata kama hataomba mchezo lakini atakuwa akijisikia raha kukuona ukiwa umevaa vazi hilo huku ukizunguka hapa na pale.
Unavaa khanga moja kisha unaenda gengeni! Hivi huoni kufanya hivyo ni kuonesha usivyoujali mwili wako? Tuache ulimbukeni wa kuiga mambo yasiyofaa. Tubadilike!

www.globalpublishers.info

2 comments:

Anonymous said...

Uko ulimwengu gani ndugu yangu ! We umeolewa ! Manaake unanifaa !

Anonymous said...

Ni kweli kabisa maadili hakuna hata kidogo unakuta mke wa mtu na akiliza zake kabisa amevaa suruali,kiblouse kinapanda juu mishanga yote nje na yeye anajiinamisha kwa wanaume na watoto pia hapo ukiwa Kama mama unatoa Somo gani?kwa kweli unapenda ujana wakati umeisha ingia kwenye Ndoa na una watoto maumbo unayaacha wazi,na wakati huo mtu unakuta ajidai yeye ni mkiristu/mwisilamu safi kweli jamani tujirekebishe