Diwani wa Kata ya Gulumungu (CCM) Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Claud Masangija, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na kosa la kuchana bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Diwani huyo alihukumiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini ya Sh. 100,000 baada ya kukiri kosa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Misungwi Saidi Kasonso.
Kufuatia diwani huyo kukiri kosa lake, ndipo Hakimu Kasonso alipomtaka mtuhumiwa kujitetea kabla ya kusomewa hukumu, ambapo aliomba apunguziwe adhabu kwa vile alifanya kosa hilo wakati akiwa hajitambui (amelewa).
Hata hivyo licha ya utetezi huo, Hakimu Kasonso alimhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh. 100,000, ambapo mtuhumiwa alilipa faini hiyo na hivyo kuepuka kwenda jela kutumikia kifungo hicho.
Kwa mujibu wa Hakimu, kati ya fedha hizo, Sh. 75,000 ni faini ya mahakama na Sh. 25,000 ni fidia ya bendera ya Chadema pamoja na mlingoti ambavyo aliviharibu.
Mwendesha Mashtaka, Theophil Lucas, alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Desemba 27, mwaka jana na kuwa siku hiyo saa 10:00 jioni, mtuhumiwa alifika katika kijiji cha Chabusongo na kuchana bendera ya Chadema pamoja na kuvunja mlingoti wake.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment