Liberatus Mwang'ombe, aliyekua katibu wa muda CHADEMA DMV
Moja: Uwazi wa mishahara ya wanasiasa
Katiba mpya iruhusu kuweka wazi mishahara ya wana siasa na marupu rupu yao (pamoja na Rais). Viongozi wa nchi ni waajiliwa wa wananchi, hivyo basi ni haki ya muajili kujua anamlipa muajiliwa wake kiasi gani.
Pili: Adhabu ya kifo
ADHABU YA KIFO ifutwe. Kwa jinsi dunia inavyoendelea kisayansi na technologia kuna uwezokano mkubwa mtu kuonekana na hatia leo na kuhukumia kifo na miaka ijayo kuzihilika kuwa alikua hana hatia. Mfano, mtu huyo ananyongwa baada ya kukutwa na hatia. Baada ya miaka kumi (kunyongwa) kutokana na kukua kwa sayansi na technolojia inagundulika kuwa mtu aliye nyongwa hakua na hatia. Tutawezaje kumrudisha? Tumeona mifano mingi kwenye nchi zilizo endelea, watu wapo kwenye “death row” lakini DNA imekuja kuwatoa kwenye hatia baada ya miaka mingi kwa ajili ya kukua kwa sayansi na technologia.
Tatu: Umri wa kugombea nafasi
Umri wa kugombea nafasi za uongozi ushushwe (pamoja na Uraisi). Kama mtu wa miaka 18 au 21 anaweza kuchagua kiongozi, kutumika jeshi au polisi, ni haki kuwa na HAKI ya kuchaguliwa kutumikia ofisi yoyote ya serikali.
Nne: Uraia pacha
Kwa jinsi dunia inavyo badilika, sasa ni muhimu kuruhusu uraia pacha. Tanzania tupo katika nchi za Africa mashariki, Kenya na Uganda. Wenzetu hawa wamesha ruhusu uraia wa nchi mbili, hii inawapa nafazi zaidi kuwa washindani katika level ya kimataifa kuliko sisi. Tunahitaji hili ili tuweze kuwa na nafasi sawa na wenzetu wa Afrika mashariki na dunia kwa ujumla. Tunaweza kutengeneza misingi kwenye katiba yetu ambayo itakuwa vigumu kwa wageni kuchukua uraia wa nchi yetu. Mfano, mtu hawezi kuwa raia wa Tanzania hadi awe ameishi Tanzania kwa miaka ishirini na asiwe amevunja sharia yeyote ya nchi. Pili, mtu anaweza kuvuliwa uraia kama atavunja sharia za nchi. Au, tunaweza kuweka sharia ya kuto toa urai kwa wageni na Mtanzania yeyote mwenye uraia wa nchi nyingine akiwa Tanzania ni lazima afuate sharia za nchi hadi pale atakapo toka nje ya mipaka na atachukuliwa ni mtanzania wa KUZALIWA. Kumbuka, waTanzania wanao chukua raia nyingine ni waTanzania wa kuzaliwa, mioyo yao ni Tanzania, majina yao ni Tanzania, ndugu zao ni waTanzania, wanaipenda Tanzania, na wanazungumza Kiswahili, isipo kuwa sio waTanzania kwenye makaratasi. Achilia mbali mchango wao kwa Taifa.
Tano: Viti maalumu
Viti maalumu viondelewe kwenye katiba. Viongozi wanapaswa kuwawakirisha wananchi, hivyo basi inapotokewa kiongozi anateuliwa na Raisi anakuwa ana kila sababu ya kutetea maslai ya aliye mteua (Raisi) badala ya wananchi.
Sita: Madaraka ya raisi
Raisi asiruhusiwe kuchagua wakuu wa mikoa bali apewe madaraka ya kuchagua baraza lake la mawaziri ambalo wachaguliwa wasiwe wabunge. Pia, wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi badala ya kuteuliwa na Raisi. Napendekeza kipindi cha ukuu wa mkoa kiwe cha miaka sita, lakini unaweza kutumikia vipindi visivyo na ukomo kama ukiwa unachaguliwa kila mara.
Saba: Rasilimali
Rasilimali za madini, mafuta gesi n.k ni mali ya waTanzania. Hivyo basi, serikali kabla ya kusaini mkataba wowote ni lazime upitiwe na bunge.
Nane: Mamamlaka ya bunge
Bunge kama mwakilishi wa wananchi liwe na HAKI ya kumuwajibisha au kumfukuza kazi Raisi endapo atatumia madaraka yake vibaya. Pia Raisi asiwe na kinga zidi ya sharia akiwa madarakani au baada ya kumaliza uongozi.
Tisa: Elimu na Afya
Elimu na Afya iwe ni haki. Katiba iidhinishe kuwa ni HAKI kwa kila mtanzania kupata matibabu anavyo kuwa mgonjwa na pia ni haki kwa kila mtanzania kupata elimu. Matibabu na elimu visiwe bidhaa au biashara. Hivi viwe basic “ HUMAN RIGHT” kama haki ya KUISHI.
Liberatus Mwangombe.
4 comments:
kaka ,kidogo umejaribu kuchangia mawazo ya wengine,hakuna jipya lolote ulilolizungumzia zaidi ya kurudia yaliyosemwa na viongozi wa juu wa vyama vya siasa tanzania.kuhusu adhabu ya kifo hata nchi zilizoendelea unapocommit capital crime(masacre)unakuhukumiwa kunyongwa,mfano watu wanacommit genocide kama ya rwanda au sudan unataka wasiuwawe?!! kuhusu mishahara ya mawaziri na raisi mbona iko wazi inajulikana,labda huijui katiba ya nchi hilo ni mojawapo ya suala liko bayana ndani ya katiba yetu. umri wa nafasi ya kugombea uongozi umeshauri uwe kati ya miaka 18 au 21!!! hivi wewe ndugu hujui kuwa huo ni umri wa wanafunzi bado wako vyuoni!!!! halafu unasema dunia ya sasa inaendeshwa na teknolojia,sasa kama unaamini hivyo kwa nini nchi iongozwe na viongozi sio wasomi!!! nafikiri ni vizuri ufanye uchambuzi kabla hujachangia mada. uraia pacha,unachanganya mambo!!unashauri eti wapewe utanzania waliozaliwa tanzania.!! kuwa raia wa nchi nyingine ni lazima uonyeshe kimsingi utaleta maedeleao gani katika taifa hilo sio kuapply tu,kiuchumi ni mtanzania gani wa pato la kati(middle class) anaweza kushindanishwa kiuchumi la raia wa marekani au norway wa pato la kati(middle class). hiyo ni moja ya sababu ya kimsingi kwa nini tanzania haipo tayari kwa uraia pacha>sio kwa ajili ya kusafiri huwa tunaangalia kiuchumi itamsaidia hivi mtanzania wa kati. wakuu wa mikoa:hujatupa sababu za kimsing kwa nini wasiwe na kikomo!!! elimu na afya tayari ipo katika katiba ya nchi yetu ni haki ya msingi wa kila mtanzania,usichanganye mambo kama haki hiyo ya msingi haipatikani basi viongozi wetu wameivunja katiba,ni vizuri ukasoma katiba ya tanzania. halafu unazungumzia suala la rais kuondolewa kinga akishamaliza muda wake!!! cha msingi hapa sio kinga ndio suluhisho. rais asiwe juu ya katiba hilo ndio suluhisho,tayari tuna branch tatu(judiciary,legislature na executive) ushauri wa bure ndugu soma katiba acha kusikiliza wanasiasa>
Anonymous wa kwanza mbona unatoka povu. Sasa si na wewe uchangie kama mwenzako kakosea? Eti unakuja Anonymouos kuchangia... MAJUNGU.
Kamanda wa kwanza, naona umejitahidi sana kunivuta sharubu. Huu ni wakati wako na ulivyo kuwa mtu wa majungu unakuja anonymous. Nilitaka nisikujibu kwa kua naona haya ni kama majungu (anonymous), lakini nimeona nisipo fanya hivyo nitakuwa nainyima HAKI ya information jamii yangu kwa upotoshaji na ukatishaji tamaa wako kwa watu wengine wanao taka kuto mchango wa katiba.
Nazani umesahau msingi wa kuchangia katiba. Ni kwamba katiba inaundwa (inabadirishwa), kwa hiyo, kama nachangia kitu ambacho kipo kwenye katiba sioni tatizo kwani kuna uwezekano wa kitu hicho kutolewa na mimi nataka kiendelee kuwepo. Pili, swala la adhabu ya kifo, nadhani unapata taabu kuelewa mchakato wa katiba mkuu. Kila mTanzania ana HAKI ya kuchangia anavyo ona ni sahihi, mimi mtazamo wangu adhabu ya kifo ni UNECTHICAL na sio sahihi. Hata kama uliua, achilia mbali science ije ikutolee makosa baadaye. Hii ina tokana na beliefs na information nizlizo nazo. Wewe pia una kila sababu ya kuamini kuwa adhabu ya kifo ni sahihi.
Tatu, ume criticize mchango wa umri wa kugombea kwa hoja dhaifu kuwa hiyo ni miaka ya uanafunzi, katiba ya Tanzania haibagui mtu kwa miaka, dini au kabila lake. Again-haya ni mawazo yangu ingekuwa vema na wewe utoe yako. Swala la uraia wa nchi mbili, nimeto sababu na nikasema achilia mbali mchango wa diaspora kwa taifa, fedha na mawazo. (FYI, diaspora wametuma more than $350 millions in 2011, fedha ambayo ni nyingi ya kigeni kuliko ya chai, pamba na kahawa kuchanganya- sawa na 5% ya fedha za kigeni zilizo ingizwa mwaka huo). Pia, sheria za immigration zina mbana mwanamke, mfano, mwanamke akiolewa na mgeni anapoteza uraia wa Tanzania na hawezi kumfanya mume wake raia wa Tanzania. Wakati mwanaume anaweza kufanya hayo. Kwa mtazamo wangu urai pacha uta suruhisha hili. Inaonekana hujaelewa kabisa nilicho kisema juu ya uraia pacha kwa hiyo sita enda huko sana.
Swala la AFYA, katiba ya nchi haisemi kuwa afya ni HAKI ya kila mTanzania. Na kwa taarifa yako Neno AFYA kwenye katiba ya sasa lime tajwa mara mbili tu kwenye katiba, Page 31 “ Mkutano wa baraza la mawazi….hali ya AFYA ya Raisi utahesabiwa kuwa mkutanao halali…” Haiongelei kuwa AFYA ni haki ya kila mtanzania wala raisi. Pia page 23 Sheria ya 1994 Na.34 ib.6 (b) neon afya limetajwa pia lakini haliongelei kuwa Afya ni HAKI ya kila mTanzania. Mwisho, sitaendelea kukuelimisha kwa kuwa unakuja kama anonymous, ungekuwa una hoja ya kujenga ungekuja na identity halali. Sirudi tena hapa.
For your benefit, utapata katiba ya Tanzania hapa: http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf
lol,acha kurudia porojo za viongozi wa kisiasa.katiba haujui,haina maana neno afya lazima litajwe mara nyingi ndio limake sense. huna haja ya kunielimisha katiba,katiba najua vizuri ila usiwe mbadala wa viongozi wa kisiasa.
Post a Comment