ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 16, 2013

Polisi waua watu watatu Muleba

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera wakati wakirushiana risasi na askari polisi baada ya watu hao kujipanga kuvamia kituo cha mafuta cha Beach.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi, alisema watu hao waliuawa juzi saa 2:15 usiku, baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kuna watu wamejipanga kuvamia kituo hicho cha mafuta kilichopo karibu na kambi ya Wachina.

Alisema polisi waliweka mtego na majambazi walipofika kwenye kituo hicho kabla ya kufanya uhalifu huo waliamriwa kujisalimisha, lakini walikahidi amri hiyo na kuanza kufyatua risasi na kuwalazimisha polisi kujibu.

Kwa mujibu wa Kamanda Kalangi, majambazi wawili walikimbia na kuelekea kusikojulikana, na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea.

Kalangi alisema mmoja wa watu waliouawa mfukoni mwake alikutwa na kitambulisho kinachomtambulisha kwa jina la Japhet Mwigabo, mkazi wa Kirundo, Burundi.
CHANZO: NIPASHE

No comments: