ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 15, 2013

WEMA SEPETU AZUA KIZAAZAA

KATIKA hali isiyo ya kawaida ya kutozea maisha ya kijijini, msanii asiyeishiwa matukio, Wema Sepetu, hivi karibuni alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuwakumbatia wazee wa kijijini baada ya kukimbia panzi, pindi walipokuwa katika ziara ya uzinduzi wa mpango wa Kilimo Kwanza kwa vijana eneo la Kwandelo, Kondoa. Hali hiyo ilimtokea mara kwa mara na hakuwa na njia nyingine zaidi ya kukimbilia kwa wazee ambao, walionekana kumcheka. Wakati wakiwa katika harakati za kuhamasisha, panzi alianza kuruka ruka eneo hilo ambalo ni sehemu ya shamba hali iliyomchanganya msanii huyo na kuanza kukimbia hovyo huku akijifunika usoni na mkoba wake akimbilia sehemu waliyokuwa wamesimama wazee. Mmoja wamashuhuda alisema Wema alikuwa akishtuka kila anapomwona Panzi, kwani ilikuwa lazima wasanii hao waingie shambani kuoneshwa mfano wa vijana kuhusu Kilimo Kwanza. Hata hivyo baada ya kurejea Dar mwandishi wa DarTalk alizungumza na mrembo huyo ambapo alisema kuwa hakuwahi kumuona mdudu huyo hivyo hali hiyo ilimpa wasiwasi mkubwa kwa kuhisi anaweza kumfanyia kitu mbaya kwa afya yake kwani walikokuwa ni kijijini sana.

No comments: