Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib (kulia)'Diamond Plutnum', akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi R.I.P..........KIDUDE BINTI BARAKA
Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu bi Kidude, Zanzibar
Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi)
Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude
Guru G na Mh Bhaa mazikoni
Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude
Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani
1 comment:
inna lillahi waina illahim rajiun rahman amlaze mahali pema peponi am ghufiriye na sisi tuliobaki its a learn and lesson duniani tunapita njia ni transit mwisho wa safari ya mtu ndo hii tukitaka tusitake so tuwe waja wema tutende mema, tumuogope mola wetu kwa sababu kuna siku tutakuja kukutana naye na kuhukumiwa kwa yale tuliyo yatenda hapa duniani.
so tujaribu sana kuwa waja wema na kutendeana wema hapa duniani na kuoneana huruma na imani
NY
Post a Comment