ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 14, 2013

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuwaonesha wasanii Aprili 24. Star Light Hotel bure

Peter Mwenda
SHIWATA imeandaa maonesho maalum kila mwezi ili kutoa nafasi kwa wasanii wa fani ya mbalimbali pamoja na wanamichezo kuonesha vipaji vyao.
Wasanii wengi chipukizi wanakosa mahali pa kuonesha kazi zao, mara nyingi kazi za wasanii wakubwa ndizo ambazo hurushwa katika redio na luninga (TV).
SHIWATA imeamua kuandaa maonesho haya kwa malengo makuu yafuatayo
(1) Kukuza vipaji
(2) Kuwapatia soko (underground) mahali ambapo wanaweza kuonesha vipaji vyao na kuwashawishi mapromota mbalimbali kuwaajiri.
(3) Kuelimisha jamii kuhusu matatizo mbalimbali kama maadili na magonjwa kama UKIMWI,malaria.
(4) Kuimarisha umoja kati ya wasanii na wanamichezo
SHIWATA inawataarifu viongozi mbalimbali na makundi ya sanaa na Michezo pamoja na wasanii binafsi kutakua na mkutano Siku ya Jumatano Aprili 17 mwaka huu saa 8 mchana katika ukumbi wa Splendid,Bungoni Ilala kupanga ratiba na kupata taarifa zaidi.
Onyesho la Kwanza litaoneshwa katika ukumbi wa Star Light Hotel, Mnazi Mmoja Dar es Salaam siku ya Jumamosi Aprili 24.
Michezo itakayoneshwa ni pamoja na maigizo, sarakasi, ngoma, kwaya, karate, Taekwondo, Taarab, Dansi, Bongo Flava, Mavazi, Gospal na Kasida, mada kuu katika maonesho hayo ni Amani na Utulivu.
Hii ni nafasi ya pekee kwa wasanii chipukizi (underground) kuonesha vipaji vyao.Watengenezaji wa filamu, mapromota, wamiliki wa bendi, MaDj na wanunuzi wa mbalimbali wa kazi za sanaa wanaalikwa ili waweze kuona vipaji na kununua kazi za wasanii hao chipukizi.
Wanafunzi wenye vipaji kutoka shule za msingi, Sekondari na vyuo mbalimbali wanaalikwa kuja kuonesha vipaji vyao.
Mipango iliyofanywa ili maonesho haya yarushwe live kituo kimojawapo cha televisheni.
Kutokuwa na chakula kwa wasanii na zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa wasanii watakaofanya vizuri katika kila onesho.
Hii itakuwa nafasi nzuri kwa wapenzi wa burudani ya sanaa kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajui wapi wanaweza kupata burudani kama hiyo kiingilio kitakuwa bure.

Wote mnakaribishwa

Peter Mwenda 0715/0752- 222677
Ofisa Habari wa SHIWATA

No comments: