Mkurugenzi wa Rodgers Export LLC ya North Carolina, Haji Abdullah akimkabidhi Dj Luke mchango kutoka katika kampuni hiyo ya usafirishaji mizigo kutoka Marekani kwenda Tanzania. Mchango ni wa kusaidia maandalizi ya sherehe ya miaka mitatu ya Vijimambo, itakayoambatana na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili litakalo wajumuisha Maprofesa wanaofundisha Kiswahili kutoka vyuo mbalimbali hapa Marekani na nyumbani, Mitindo ya Mavazi kutoka Tanzania na hapa Marekani, wasanii mbalimbali ndani na nje ya Marekani, na mambo mengine mengi katika ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Jumuiya ya Watanzania DMV.
No comments:
Post a Comment