ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 15, 2013

Wenye malori Tanzania wailalamikia Zambia

Dar es Salaam. Chama cha Wamiliki wa Malori ya Usafirishaji Mizigo Tanzania (Tatoa) wameilalamikia Serikali ya Zambia kwa kuruhusu Mji wa Mbala nchini humo kuwatoza Dola 50 za Marekani sawa na zaidi ya Sh80,000 kwa maegesho ya lori moja kwa siku wakati madereva wanashughulikia taratibu za kutoa nchini humo.
Kimesema kitendo hicho ni kikwazo kwa maendeleo ya uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Zambia na kwamba kinavunja mikataba mbalimbali ya kibiashara kwa Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc). Tanzania inatoza Sh3,000 za maegesho kwa siku.
Kauli hiyo aliitoa msemaji wa Tatoa, Elias Lukumay kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu , Omary Kiponza alipozungumzia kero zinazokwamisha sekta ya usafirishaji wa mizigo nchini na nchi jirani.
“Uongozi wa Tatoa ulishawasilisha malalamiko haya kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ambaye tunaamini anaendelea kuwasiliana na uongozi wa Zambia ili kuondoa kero hiyo’’alisema. Habari kutoka Wizara ya Uchukuzi zilithibitisha juzi kuwapo kwa mazungumza hayo na kwamba ufafanuzi utatolewa baadaye.
Lukumay alizungumzia pia kero ya Tanroads kuyakamata malori yanayoegeshwa kando ya barabara ya Mandela na nyinginezo jijijini Dar es Salaam kwamba tatizo ni kuwapo kwa vituo vingi vya kutunza makontena (Inland Container Deport) katika maeneo hayo.
Kuhusu suala la mizani ya kupima malori, Lukumai aliisihi Serikali isikikilize ombi la Tatoa kutaka mizani iwepo bandarini ili malori yanye mizigo yapimwe kabla hayajaanza safari ya kuelekea mikoani ama nje ya nchi.
Alisema inasikitisha kuona lori linapakia mzigo mzito bandarini bila kupimwa na linakamatwa nje ya bandari.
Mwananchi

No comments: