Meneja wa shirika la Tanesco mkoa wa mbeya Mhandisi Simon Maganga akiongea na waandishi wa habari juu ya wizi wa umeme kwa wateja ambao sio waaminifu
Mafundi wa Tanesco wakimweleza meneja wao jinsi mteja alivyojiunganishia umeme wa wizi maeneo ya sae mbeya
Hivi ndiyo mwenye nyumba alivyojiunganishia umeme wa wizi katika nyumba yake
Hii ndiyo gari inayotumika na mafundi wa Tanesco kupita nyumba hadi nyumba kukagua mita zao kama zimechezewa na kulitia hasara shirika hilo
Zaidi ya shilingi milioni 50 zimetajwa kupotea katika shirika la umeme tanesco mkoani mbeya kwa kipindi cha miezi 3 kufuatia kuibuka kwa wimbi la wizi wa mafuta ya transifoma pamoja na wizi wa vifaa vingine .
Meneja wa shirika hilo mkoa wa mbeya Mhandisi Simon Maganga amesema kuna tatizo kubwa la wizi wa transifoma na mafuta yake pamoja na vifaa vingine ambavyo thamani yake inakadiliwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 50 vimeibiwa katika kipindi hicho .
Amesema suala la wizi limeibuka upya ambapo baadhi ya wananchi wasio kuwa waminifu wamekuwa wakifanya vitendo hivyo hasa kwa maeneo ya wilayani ambako ndiko wizi huo umekuwa ukifanyika marakwa mara.
Kufuatia hali hiyo tayari shirika hilo limekwisha patiwa vifaa ambavyo vitaweza kuwasaidia katika msako huo wa kuwakamata wahalifu wanao lihujumu shirika hilo.
Moja ya vifaa vipya vilivyotolewa na serikali katika kukabiliana na tatizo hilo Mhandisi Maganga amesema kuwa ni pamoja na vyombo vya usafiri ambavyo teyari wamekwisha patiwa gari jipaya aina na Toyota Landcruse ambayo itawalahisishia kufika maeneo mengi zaidi .
Hata hivyo Meneja huyo amesema kuwa kutokana na msako waliokwisha kuanza wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya wahalifu wanaolihujumu shirika hilo na wanatalajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.
Ametaja baadhi ya wilaya ambazo zimekuwa vinara wa wizi huo amabyo ni pamoja na Halimashauri ya wilaya ya Mbarali pamoja na Mbeya mjini ambapo Apri 12 mwaka huu walifanikiwa kumakata mkazi wa eneo la Sae Ndugu Saimon Chengula mara baada ya kujonganishi umeme kinyemela.
Kufuatia hali huyo ametoa wito kwa wananchi jijini humo na maeneo ya irani kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa viongozi wa shirika hilo kwa wale ambao wamekuwa wakilihujumu shirika hilo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Mbeya yetu
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment