Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Kaimu Mkuu wa hifadhi ya Mikumi,Bwa.Datomax Selanyika wakati alipokuwa akimuelezea faida za kuhifadhi Mbuga za Wanyama na kutunza maizngira ya Mbuga hizo,aidha pia Dotomax alizungumzia mipango na mikakati ya kuihamisha barabara ya lami itokayo Dar kuelekea Tunduma ambayo imekatiza ndani ya hifadhi na alifafanua pia kuhusiana na faida ya kuihamisha barabara hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na Wananchi wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kilosa Town.Kinana alikuwemo Wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha chama na kukagua miradi mbalimbali ya chama hicho.
Katibu wa NEC Itikadi na Ueneze-CCM,Nape Nnauye akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kilosa Town,Nape aliawasa wakazi wa Kilosa kuwa makini na mambo ambayo wamekuwa wakiambiwa kutoka kwa vyama vingine ambavyo vimekuwa vikipotosha ukweli wa mambo kuhusiana na mambo mbalimbali yanayowahusu.
No comments:
Post a Comment