ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 16, 2013

HAPA NA PALE KATIKA HABARI

Gorofa linalojengwa katika eneo la Ilala Bungoni mtaa wa mafuriko jijini Dar es salaam bila kufuata sheria ya kuweka vizuizi kwa ajili ya usalama wa watu, imesababisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka 6 baada ya kupigwa na mbao yenye misumari iliyorushwa kutoka juu ya gorofa hilo na kufariki papo hapo.
-----
Rais Jakaya Kikwete amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uongezwaji wa virutubishi zaidi kwenye bidhaa za vyakula ambapo amesema serikali imekuwa ikipambana na tatizo la utapiamlo tangu uhuru lakini bado halijaisha na kuongeza kuwa uelewa mdogo wa jamii juu ya masuala ya lishe,mila na desturi potofu kwa baadhi ya jamii vimekuwa tatizo kubwa katika mapambano dhidi ya tatizo hilo.
-----
Serikali imeshauriwa kuongeza juhudi za utoaji wa taarifa za rasimali za gesi na nishati mbalimbali kwa wananchi, baada ya Tanzania kushika nafasi ya 27 kati ya nchi 58 za Africa katika usimamizi na utawala wa rasilimali hizo katika ripoti iliyotolewa na taasisi ya utafiti ya Revenue watch.
-------
Baadhi ya wapenzi wa timu wa Simba kisiwani pemba wamesema hawatishwi na kambi ya Yanga kisiwani hapo kwani mazoezi yao walio yaona ni yakawaida huku uongozi wa Yanga ukielezwa kushangazwa na wapinzani wao Simba kulalamikia muamuzi.
Chanzo:ITV.

No comments: