Diwani Athuman. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, jana alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku, baada ya wanafunzi waliosimamishwa masomo kuwahamasisha wenzao kupinga adhabu hiyo na kufanya vurugu. Alisema tukio hilo limesababisha uharibifu mkubwa wa mali za shule hiyo ingawa moto huo haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu. Akisimulia tukio hilo, Kamanda Diwani alisema chanzo ni wanafunzi watatu wa shule hiyo kusimamishwa masomo utokana na utovu wa nidhamu. Alisema wanafunzi hao baada ya kusimamishwa masomo walianza kuwahamasisha wenzao kuwaunga mkono katika kupinga adhabu hiyo, jambo lililopelekea kufanyika kwa vurugu kubwa shuleni hapo.
Alisema bweni lilichomwa moto lilikuwa ni la wanafunzi zaidi ya 50 ambao hawakuwa tayari kuwaunga mkono wanafunzi hao, hali iliyosababisha wenzao kulichoma bweni walilokuwa wakilala.
Kamanda Diwani alisema jumla ya wanafunzi 15 wakiwemo waliokuwa wamesimamishwa masomo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Rungwe kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na vurugu hizo.
Alisema tathimini ya uharibifu wa mali bado inaendelea kufanywa ili kujua thamani ya mali iliyoharibiwa na moto huo.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment