Wednesday, June 12, 2013

INGAWA INARAHISISHA USAFIRI LAKINI PIA INARAHISISHA KUFUPISHA MAISHA YA MADEREVA NA ABIRIA WAKE BODA BODA HIYO

Wakazi wa Ukonga Mazizini Wilayani Ilala jiji la Dar es Salaam wakipita kando ya pikipiki iliyo lala chini baada ya mwendeshaji wake kugonga gari aina Hice mapema asubuhi ya leo kufuatia dereva wa Hice kukata kulia bila ishara.
Dereva wa bodaboda shsti ya njano akijadiliana na dereva wa Hice (fulana ya pink) aliyemchomekea ghafla. Dereva huyo wa Hice alichapwa makofi kadhaa na mashuhuda wa ajali hiyo.
Dereva wa bodaboda akinyanyua pikipiki yake baada ya kupigwa kikumbo na gari dogo leo katika barabara ya Mandela eneo la Tazara. Abiria wake alishtuka mguu kidogo lakini badae waliendelea na safari.
Abiria wa bodaboda (mwana dada dera la njano) akiwa na wasamaria wema mara baada ya ajali kutokea nae akiwasilina na marafiki zake kuwa kakoswa koswa na gari.
Hii ndo gari iliyowa piga kikumbo.

No comments: