MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama Wilfred Lwakatare amejitokeza adharani na kumvaa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba Lwakatare alipokuwa Chama Cha Wananchi (CUF) hakufundishwa ugaidi.
Lwakatare ambaye aliachiwa uhuru kwa dhamani hivi karibuni baada ya kukaa mahabusu kwa siku 92, alimshambulia Mtatiro katika waraka wake mrefu ambayo nakala yake imenaswa na mtandao wa Habarimpya.com, alisema kwamba hakuelewa maana ya maneo hayo ya Mtatiro aliyoyatoa mbele ya Waandishi wa Habari wakati akiwa mahabusu.
"Nikiwa Gerezani Segerea nilimshangaa sana ‘bwana mdogo’ Julius Mtatiro- alipozungumza kwenye vyombo vya habari kuwa ”Lwakatare akiwa CUF hatukumfundisha ugaidi.”
Sikumuelewa hayo maneno alikuwa na maana gani na alitumwa na nani"alisema Lwakatare na kuongeza.
"Kwanza sijui kipindi hicho nikiwa CUF yeye alikuwa wapi na sidhani kama kwa wakati huo alifikiria hata kujiunga na hiyo CUF.
Awaulize CUF ‘Original’ kama wapo, Lwakatare alikuwa ni nani ndani ya CUF".
Lwakatare katika wakaraka huo alifafanua kwamba hata siku moja haitatokea akabeza uzoefu na msingi wa kisiasa alioujenga ndani ya akili yake na nafsi yake kutoka CUF, na kwamba CUF ilimweka katika ramani ya kisiasa anayoitumia kutamba nayo hadi leo hii.
"CUF ilinijengea nguzo moja kubwa iliyonipaisha kisiasa na inayoendelea kunisaidia katika kazi niliyokabidhiwa Chadema ya ulinzi wa chama hadi leo, ambayo ni ujasiri, kujitoa kwa nafsi yangu na kwa akili zangu zote kuipigania na kuitafuta haki bila kuchoka na kutokukubali dhuluma na uonevu, haki huwa huletewi kwenye kisahani cha kikombe cha chai, haki hudaiwa na kutafutwa.
No comments:
Post a Comment