MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha kufikiria kuachana na kazi hiyo.
Akichonga na paparazi wetu pasipo kuwataja ‘wabaya’ wake, Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’ za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.
“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali ni tete,” alisema Shilole.
1 comment:
Dada sio wasanii tu maana hata hapa marekani Kulogana kumepamba moto yaani ni Hatari tupu maana kuna wanaoenda kwa waganga wa Kihaiti wengine Wawest yaani tabu tupu. Endelea kumuweka mungu mbele hayatakupata mabalaa yao.
Post a Comment