Wednesday, June 12, 2013

MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHURI

Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Wabunge, wakikagua jezi zao baada ya kukabidhiwa.

No comments: