Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi
Alisema hayo jana Bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza, ambapo alisema kwa muda mrefu wabunge wengi hasa wa CCM wamekuwa wakilalamika kwamba ahadi nyingi zinazotolewa hazijatekelezwa.“Mheshimiwa Spika hata katika kile kipindi cha kwanza kuna ahadi ambazo hazijatekelezwa. Je, hatuoni sasa kuna sababu muhimu ya kuhakikisha kuwa Marais wanapotoa ahadi na wanamaliza vipindi vyao bila ahadi hizo kuzitekeleza wanapelekwa mahakamani?” alihoji mbunge huyo.
Akijibu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema Marais wamekuwa wakikitoa ahadi kwa namna mbalimbali.
“Kuna ahadi za msingi zilizopo kwenye Ilani lakini pia zipo ahadi ambazo binadamu yeyote akifika mahali hata wewe (Mbunge) huwa unaahidi kutokana na hali uliyoikuta…inafika mahali unajikuta lazima utoe ahadi,” alisema.
Hata hivyo, alisema serikali ya CCM imekuwa ikijitahidi kutekeleza ahadi hizo.
“Na Rais akishatoa ahadi…ahadi hiyo itatekelezwa kwa fedha za serikali na si kwa fedha za Rais” alisema.
Alisema kama serikali itaweza kwa wakati huo kutekeleza ahadi jusika itafanya hivyo na ikishindwa itatoa maelezo kwa kuwa ahadi hizo ni endelevu kwani anapoingia Rais mwingine atazitekeleza.
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Mkinga, Dunstan Kitandula (CCM), alitaka kujua ni hatua gani zimechukuliwa hadi sasa katika utekelezaji wa ahadi za kujengwa hospitali ya wilaya ya Mkinga na kukipandisha hadhi kituo cha Afya cha Maramba ili kitoe huduma za hospitali ikiwemo upasuaji.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi alisema katika kutekeleza ahadi hizo, serikali imetumia Sh. Milioni 132.1 kuboresha miundombinu ya kituo cha Afya cha Maramba ili kiweze kupandishwa hadhi na kutoa huduma zinazokaribia huduma za hospitali.
Kuhusu ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Mkinga, alisema serikali imekwishatoa Sh. milioni 221.4 ambapo Sh. milioni 21 zimetumika.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Well, that is why we call home grown "Politicians". In some instance, they keep 20% what they promise, and the rest 80% they hold as a promise for the next elections. In think people should switch to electing "engineers"
Engineers will build the bridges they promised-eventually on time
Post a Comment