Stori:Musa Mateja
JENGO lenye gholofa 15 lililojengwa kwenye Barabara ya Barack Obama, hatua chache kutoka kwenye Ikulu ya Tanzania jijini Dar es Salaam limeshangaza wengi baada ya waliodaiwa kutoa kibali cha ujenzi kupandishwa mahakamani Jumatano iliyopita.
Jengo hilo lililopo hatua chache kuifikia Hospitali ya Ocean Road limezua maswali mengi kutoka kwa wakazi na wafanyakazi wa mitaa hiyo baada ya ujenzi huo kumalizika na ndipo serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa nchini (Takukuru) ikawapandisha kortini wahusika.
Inadaiwa kuwa, kwa kawaida serikali hairuhusu kujenga majengo marefu umbali wa mita mia kutoka ikulu. Jengo hilo linadaiwa kujengwa ndani ya mita 100 kutoka ikulu.
WALIOPONZWA NA KUTOA KIBALI CHA UJENZI
Jumatano iliyopita, Mtendaji Mkuu na Msanifu Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar wakikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa vibali hivyo.
Maofisa hao ni Makumba Kimweri (Mtendaji Mkuu) na Richard Maliyaga (Msanifu Mkuu) walifikishwa kortini hapo na kusomewa mashitaka yanayowakabili na Wakili wa Serikali, Leonard Swai mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Sundi Fimbo.
Swai alidai mahakamani hapo kuwa Agosti 6, 2007 Kimweri akiwa Mtendaji Mkuu wa TBA kwa kutumia vibaya madaraka yake alisaini hati ya makubaliano yenye namba TBA/JVA/DSM/ROI/001 kati ya TBA na Kampuni ya Royalle Orchard Inn Ltd akiwa na lengo la kuanzisha ujenzi na wamiliki binafsi wa umma wa ghorofa 15 kwenye Kitalu namba 45 Mtaa wa Chimara, Wilaya ya Ilala bila eneo hilo kufanyiwa upembuzi yakinifu.
WENGI WALIKUWA WAKIJIULIZA KABLA YA WAHUSIKA KUSHTAKIWA
Upo ushahidi mkubwa kwamba, hata kabla ya Takukuru kuchukua hatua hiyo, wakazi wa Jiji la Dar waliokuwa wakupita eneo hilo, swali lao kubwa lilikuwa: Hivi ni kwa nini jengo refu kama hilo limejengwa jirani na ikulu?
Swali hilo lilikosa majibu hadi Jumatano iliyopita ambapo Takukuru iliwafikisha kortini maofisa hao wa TBA.
5 comments:
Wanaoshangaa ghorofa karibu na ikulu wasubiri kushangaa ghorofa ndani ya ikulu.
Tanzania kweeli tunaelekea pabaya sana yaani sekta ya ujenzi ni sifuri kabisa haina maana hata kidogo, miezi ya nyuma tumeona jingo limeanguka na kuua watu, kitu ambacho kilitakiwa kukaguliwa kabla gorofa haijapandishwa juu, sasa tena hili hapa mnatuambia limejengwa kinyume cha sharia, mlikuwa waapi nyie sekta ya ujenzi kabla hili gorora halijafikia gorofa kumi na tano???? Mnakula rushwa mpaka mnasahau kuwajibisa na mnasahau umuhimu wa kazi zenu. Hiii sekta ya ujenzi ni ya kuundwa upya kabisaaa haifai hata kidogo. Rushwa imetawala kutoa vibali bila kuchunguza na bila uhalali ilimradi mmepewa rushwa. Haya sasa libomoeni ligorofa hilo Kiswahili kirefu hatutaki kusikia. TUMECHOKA KUDANGANYWA JAMANI.
Lakini hii sio haki kabisa.hivi mpaka jengo hii linafikia hapo lilipo walikuwa wapi.?yaani hayo ni makosa yao.... huyu mjenzi atakuwa mjinga kiasi gani au kichaa wa aina gani mpaka akubali kujenga na hali akijua litabomolewa.the whole system imeoza kuanzia rais wao mpaka watendaji.hawaogopi huyo raisi wala nini
Hivi mpka huyu mtu anapewa kiwanja na kujenga wizara husika ilikuwa wapi?wengi mtajibu kuwa alihonga ndio maana aapewa hapo sasa kosa la nani aliyehonga au aliemuuzia?? amabayo ni serikali....HUYU ALIKUWA ANAPITIA WAPI NA HAKUONA HILI JENGO MAANA ANAJIFANYA NDIO KINARA WAKUBOMOA MAJENGO!!!!! AU ANABOMOA YALE THU ALIKUWA HANA MASALAHI NAYO.....kwa kweli wakilivunja itakuwa sio haki.kwanza nani anataka kufanya chochote kibaya hapo ikulu.?? watu wenyewe wlivyowaoga kama nini.wakitobolewa macho wanafyata kimya kama vile ni kawaida au ilikuwa haki yake kutobolewa macho tumeona waandishi wakitobolewa wakirudi kutoka south africa wanaufyata mkia.mm nafikiri kuna mambo muhimu ambayo yanatisha yakufuatilia kuliko hili.watu wanauliwa, wanamwagiwa tindikali nk mm nafikiri serikali haifanyi kazi yake haswa upande wa sheria ndio maana watu wanaamua kujichukulia hatua mikononi.Juzi kati wagonjwa wamelazwa nje na eti wanafanya fumigation what kind of nonsense is that?mimi nilifikiri hao wagonjwa wko pale kwasababu wanaumwa ln kavile haitoshi wanakuwa tortured.Obama kaja hapa mliweza kufanya usafi na kujionyesha picture ambayo wakati wananchi wenu wanateseka.huu ni straight up unafiki!!!!!!!
Naomba usibanie hii tafadhali
Mdau Robert canada
Muda wote huu mlikuwa wapi mpaka gorofa limefika hatua hii. Huu ujinga wa taasisi za Tanzania ni hatari sana kwa usalama wa taifa hili letu.
Someone must lose his job sooner rather than later otherwise we are destined to fail due to our foolish schemes
Tatizo la Tanzania sio RUSHWA WALA WATOA RUSHWA . Tatizo ni Sheria za Nchi MBOVU. Sheria ya Tanzania itakwambia. Mfano. NIMARUFUKU KUKOJOA HAPA. NCHI NYINGINE WANGEWEKA HIVI. Nimarufuku kukojoa hapa adhabu ya Tsh 200, 000 au jela miaka 2 itakuangukia.Nimuda sasa kubadilisha Sheria nyingi za kikoloni kwenda na wakati. Jengo lisivunjwe ligeuzwe Mali ya taifa
Post a Comment