MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania (TEF), "Absalom Kibanda" amesema zipo taarifa mbalimbali za kutaka kupotosha ukweli kuhusu yeye, lakini ukweli utabaki kuwa kweli na tukio alilofanyiwa ni la kihalifu, linalotokana na misimamo ya kazi yake.
Aidha amesema kabla ya kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya alikuwa muoga sana na kwamba hakupata kujua kama yeye ni jasiri kwa kiwango hicho.
Kibanda alisema hayo jana wakati akizungumza Dar es Salaam katika kipindi cha Jenerali On Monday na kuongeza kuwa kalamu yake ndiyo iliyomfikisha hapo na kwamba bado atajisemea mwenyewe huku akisema kweli daima.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari Limited (2006), alijeruhiwa vibaya katika mk
asa uliotokea Machi 6, mwaka huu na kumwacha na ulemavu wa jicho, kidole na mifupa kadhaa mwilini kuvunjika.
“Nilikuwa muoga sana kabla ya kupatwa madhala haya, nilikuwa nikiwaza jambo mara mbilimbili na sikupata kujua kama mimi ni jasiri kiwango hiki…kwani hata maneno ya madaktari waliokuwa wakinihudumia yalinifariji kuwa hata shinikizo la damu na sukari viko katika hali nzuri,” alisema Kibanda na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.
Alisema zipo taarifa mbalimbali za kutaka kupotosha ukweli kuhusu yeye lakini ukweli utabaki kuwa kweli na kwamba yapo mambo ambayo atayafanya tofauti na ilivyokuwa awali.
“Katika miezi mitatu niliyokuwa nikipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini zipo lugha nyingi za kishabiki ziliandikwa…ni wakati wa kuchunguza kwa kina na kusema ukweli,” alisema Kibanda na kuongeza kuwa leo (jana) ni siku 100 tangu alipofanyiwa tukio hilo, lakini hakuna aliyekamatwa wala kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment