Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ( wa nne kulia)akipata maelezo kutoka mmoja wa wafanyabiashara wa mihogo Ilala alipofanya ziara rasmi katika masoko ya Buguruni na Ilala kuangalia utofauti bei za bidhaa kabla na kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mstahiki Meya aliwaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa mbalimbali wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha Waislamu wa mkoa wa Dar kuwa na mfungo mwema na wao pia kupata Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwani watawezesha hata wale wenye kipato cha chini kumudu bei bidhaa zinazotengeneza futari. Mh. Silaa amewatembelea wafanyabiashara katika masoko kuangalia uwiano wa bei katika masoko hayo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ziara yake kwenye masoko katika halmashauri yake ya Ilala akiwa ameambatana maafisa wa mbalimbali wa Manispaa ya Ilala.
1 comment:
nonsense...waste of public funds!!.hebu niambie importance ya hii ziara?unasema usiwapandishie bei kwa kutumia vigezo vipi na sheria ipi?what actions umechukua ulipoona bei ipo juu??je Gvnt ina-subsidize gharama za vitu?kama umeona ni bei why Gvt isianzishe maduka yake iuze bei inayotaka?
J4
Ujerumani
Post a Comment