Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji
Mwalimu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira
alipomtembelea ofisini kwake mjini Kayanga mkoani Kagera kutambulisha
mradi wa Amani na Demokrasia wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa
jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na
kudumisha amani nchini Tanzania. Mradi huo utakuwa unaratibiwa na
UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa
Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akifafanua
jambo kuhusiana na mradi wa Amani kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary
Lwegasira (wa tatu kulia) namna utakavyoendeshwa kwa wakazi wa Wilaya
yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya
Karagwe Joseph Sekiku na wa pili kulia ni Mshauri wa Radio Jamii
kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu.
Picha juu na chini ni Bw. Omary Hassan
akikusanya maoni ya vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (KDVTC) kilichopo
kitongoji cha Kayanza wilayani Karagwe mkoa wa
Kagera.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana
la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan
na Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya
Karagwe Joseph Sekiku (fulana ya Blue) kwenye picha ya pamoja na
walimu na wanafunzi wa Chuo cha ufundi stadi (KDVTC) mara
baada ya kumaliza zoezi la ukusanyaji maoni kwa wananchi wa
Karagwe.
kwa picha na maelezo zaidi bofya read more
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja
wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Omary Hassan akizungumza
na uongozi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI)
kuhusiana na ukusanyaji maoni ya Utekelezaji wa Mradi wa Amani na
Demokrasia Wilayani Karagwe. Kushoto ni Mkuu wa taasisi ya PETI
Devotha Brassio na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Fravian Gedion.
Bw. Omary Hassan akizungumza na wanafunzi wa
Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na
utekelezaji wa mradi wa Amani ambapo vijana nao wanahusika katika
kujenga Amani ya nchi kwa sababu wao ndio taifa la
leo.
Bw. Omary Hassan katika picha ya pamoja na
uongozi wa taasisi ya PETI na baadhi ya wanafunzi wa taasisi
hiyo.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa
Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akikusanya
maoni kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe kufanya tathmini ya
utekelezaji wa mradi wa Amani na Demokrasia.
Kina mama nao walihusika katika kuchangia maoni
ambapo wengi wao wameomba mradi huo utakapoanza kuwepo na kipindi
maalum katika radio jamii ya wilaya ya Karagwe cha kuwaelimisha waume
zao kuhusu swala la unywaji Pombe kupita kiasi ambao unapelekea
uvunjifu wa amani katika nyumba zao.
Mashirika ya UNDP na UNESCO yameanzisha mradi wa
pamoja wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa
vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani
nchini Tanzania.
Kama inavyojulikana haiwezekani kuwa na
maendeleo bila kuwa na amani, na haiwezekani kuwa na amani bila kuwa
na maendeleo.
Kwa sababu hiyo Jumuiya ya Kimataifa inatambua
kuwa moja ya mikakati msingi ya kujenga amani ni kuwa na msingi
thabiti wa uchumi jamii.
Pia kuwezesha raia wote kuhusisha katika kutoa
maamuzi ni kuweka msimamo katika maendeleo
endelevu.
No comments:
Post a Comment