ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 18, 2013

ZBC na Ujuha wa kuondoa Tittle ya “Maalim”

30c1f084-db70-414e-8640-6dd3b1d22b4fInasikitisha sana kuona vyombo vyetu vya habari viko mstari wa mbele kuipotosha jamii badala ya kuielekeza. Zanzibar licha ya sifa kemkem ya kuwa ya mwanzo kuwa na TV ya rangi, maendeleo ya TV hii imekuwa kinara wa kuichafua na kuipoteza jamii.Zanzibar Broadcasting Corporation (ZBC) limezuwa mapya kwa kuondoa Tittle ya “MAALIM” kabla ya jina la Makamo wa Kwanza wa Rais – Maalim Seif Sharif Hamad.
Nimeuita “ujuha” kwani inavyoonekana ZBC hawajuwi maana ya neno Tittle, na ikiwa wanajuwa basi ni dhahiri kuwa hii ni chuki binafsi kwa Makamo wa Kwanza wa Rais yenye lengo la kutaka kuleta mfarakano miongoni mwa viongozi wa SUK.

Haiyumkini hata siku moja Kumwita “Seif Sharif Hamad” wakati yeye mwenye anataka aitwe “Maalim Seif Sharif Hamad” kama vile ambavyo haiyumkini kumwita “Seif Ali Iddi” wakati mwenyewe anataka aitwe “Balozi Seif Ali Iddi”, halkadhalika haiyumkin kumwita “Ali Mohamed Shein” wakati yeye mwenye anapendelea aitwe “Dr Ali Mohamed Shein”.


Tuchukulie huu ujuha wa kwanza wa kutojuwa maana ya “Tittle”, wazungu kwa upande wao wanatumia tittle chungu nzima ikiwa ni pamoja na Mr, Mrs, Miss, Mr, Dr, Engineer, Ambassador, na nyengine yoyote unayotaka mwenyewe kuitwa. Vipi leo hii tuone dhambi na karaha kwa yule anayetumia tittle ya “MAALIM” kwa kiswahili? Wakati yeye sio wa mwanzo mtangulizi wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliweza kuitumia tittle hii hii na hiyo ZBC hadi leo wanaendelea kumwita hivyo. Kwanini naye wasimwite Julius Nyerere ikesha.

Amma kwa ujuha wa pili wa kutaka kuleta mfarakano miongoni mwa Viongozi wa SUK, hili naona kama vile ZBC imechelewa. Ikiwa hawakuvua kungelikupwa, iwe maji yashajaa!!! Nashangaa. Kwa hili halimgusi wala halimtetereshi Maalim Seif Sharif.

Mwisho nimalizie lawama zangu kuzipeleka kwa Waziri anayehusika na ZBC. Binafsi sikurudhika na ujuha huu hivyo namtaka aondoke madarakani kwani hawezi na hafahamu wajibu wa kazi yake. Tukumbuke mwaka mmoja nyuma wahariri wawili waliondoshwa kwenye nyadhifa zao kwa kurusha muda mkubwa zaidi wa Maalim Seif Sharif kuliko wa Dr Ali Shein. Hivyo naye Waziri kwa hili anapaswa awawajibishe wote wanaohusika au awajibike yeye.

Ikiwa ni kuondoa Tittle basi isiondolewe tittle ya mtu mmoja tu bali kila mmoja aondolewe Tittle yake kila wakati wa matangazo.

Mzalendo

1 comment:

Anonymous said...

hivi hawa mzalendo wanaodai heshima wao wanawaandika watu kwa kuwaheshimu?, ni mara ngapi nimeona akiandikwa huyo mwalimu nyerere bila tittle yake au na wengine kama waziri mkuu mizengo pinda, rais shein balozi iddi, na wengine na wengine. sasa mkuki kwa nguruwe tu kwa binaadamu unauma? leo kuona huyu maalim wanayemwabudu hakuitwa maalim basi wote wawajibishwe, hawana maadili, hawana adabu n.k. nimesoma mara nyingi na kuona katika blog hiyo wanaruhusu watu kuwaita wengine majina mabaya na hata kuwatukana wazi wazi, na wahariri wao wala hawachuji wala kukemea tabia hizo. nawapa heko sana vijimambo ni blogi ya kistaarabu sana mko juu sana na hata wengine pia kama michuzi n.k