ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 5, 2013

RAIS KIKWETE AANZA KUWAADHIBU WANYARWANDA WALIOPO NCHINI

MWANZA. 
MAMIA ya wahamiaji haramu kutoka nchini Rwanda wakiwa na ng’ombe zaidi 900 wameanza kuondoka nchini kurejea kwao kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka waondoke Tanzania kabla ya siku 14.

Aidha, imeelezwa kuwa kumekuwapo ongezeko la askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mkoani Kagera hasa wilayani Ngara hali inayozua hofu kwa baadhi ya wananchi, huku ikiongeza msukumo kwa wahamiaji haramu kuond
oka.

Akiwa katika ziara mkoani Kagera, Rais Kikwete alitoa agizo la kuwataka wote waliokuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria waondoke mapema jambo lililotakiwa kuanza kutekelezwa Julai 29 na kukamilika Agosti 10 mwaka huu.

No comments: