Weekend vijimambo ilitimba nyumbani kwa Dr Temba pande za Brooklyn New York na kujionea jinsi gani maandalizi ya kukarabati back yard yake itakayo tumika kwa Graduation BBQ yake baada ya kupata nondo za PHD. Graduation BBQ hiyo itafanyika siku ya tarehe 17 mwezi huu wa 8 kuanzia saa kumi jioni hapo nyumbani kwake. Back yard inajengwa sakafu mpya na kufungwa taa samambamba na ujenzi wa Jiko maalumu la kuchomia nyama. Jiko hilo litakuwa bora na maalumu kwa sababu ya kuwa alijawahi kutengenezwa sehemu yeyote. Jiko hilo lime designiwa na yeye mwenyewe Dr Temba chini ya Company yake ya T.E.S.
Mafundi wakiwa kazini kujenga sakafu mpya
Sakafu ikionekana mpya na ujenzi ukiendelea.
Fundi wa umeme akifanya vitu vyake kuakikisha siku hiyo mambo yanakuwa bam bam.
Fundi akichukua vipimo tayari kuanza ujenzi wa kusimika jiko maalumu la kuchomea njama siku hiyo ya Graduation BBQ. Jiko hili litakuwa na ubora wa hali ya juu kwani litakuwa lina tumia computer maalum ya kuzua moshi usitoke njee na kuchafua haliya hewa au nyama kunuka moshi. Computer itasahidia kuweza kusafisha moshi na kuwa hewa safi, na nyama kuchomika katika kiwango cha hali ya juu.
Dr Temba akimpa maelezo baba mkwe wake juu ya jiko hilo. Jiko hilo litakuwa very scientific kutokana na jinsi alivyo design, Ni kazi ya T.E.S hiyo
Nyumbani kwa Dr Temba baada ya fundi umeme kumaliza kazi yake mwonekano wa taa kwa nnje njakati za jioni.
No comments:
Post a Comment