ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 14, 2013

KINANA: MASWA KUFAIDIKA NA MRADI WA UMEME VIJIJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na kijana Ally Emmanuel mkazi wa Maswa mkoani Simiyu ambaye Katibu Mkuu ameahidi kumsomesha kwenye chuo cha ufundi Veta.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi wakiwasili kwenye uwanja wa Madeko tayari kuhutubia wananchi.
 Kikundi cha ngoma cha Maswa kikicheza ngoma ya Bugoyangi kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Maswa kwenye viwanja vya Madeko ambapo alisema umefika wakati sasa wa kuanza kuwapima vilevi wabunge kabla ya kuingia Bungeni .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Maswa, moja ya mambo aliyosisitiza Katibu Mkuu ni mipango mizuri ya mradi wa umeme vijijini na maji.
Wakazi wa Maswa wakionekana kukunwa na Hotuba ya Katibu Mkuu.

1 comment:

Anonymous said...

Asante, mimi naona sasa viongozi mmewachoka waliowapa kura, kwani maneno mnayoongea kwenye mikutano hayaendani na kile tunachotarajia kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Swala a kupima akili ndio mnaliona leo? Huyu kijana anayepambwa kusomeshwa veta je madarasa ya chini kayamaliza au anauza mihogo na maji barabarani. Jamani tujifunze jinsi ya kuomba kura kwa wananchi kwa kueleza kile wanachohitaji, wako wengi sana wanaohitaji elimu sasa huyu mmoja inakuwaje?? Mungu tubariki Tanzania.