Ndugu, jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu Justine Mwavita Bashonga (mama yake mzazi Yves Bangonga ambaye ni Afisa Ubalozi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Marekani) kwenye Ibada ya kumuombea na kuamuaga marehemu iliyofanyika katika kanisa la St. Mary's lililopo Rockiville, Maryaland, Mwavita Bashonga alifariki siku ya Jumamosi Sept 7, 2013 kwa saratani ya ini na mwili wa marehemu utasafirishwa kesho Jumamosi na huku ukisindikizwa na watoto wa marehemu na familia zao kwa mazishi DRC.
Yves Bashonga akiwa na mkewe Latifa Bashonga ambaye ni Mtanzania kwenye Ibada ya kumuombea na kumuaga marehemu iliyofanyika Ijumaa Sept 13, 2013 Rockville, Maryland.
Kutoka kushoto ni Yves Bashonga, Latifa Bashonga, Lucien Bashonga na Toussaint Bashonga wakifuatilia Ibada ya marehemu Mwavita Bashonga iliyofanyika Rockville, Maryland Ijumaa Sept 13, 2013.
Waziri wa zamani wa Fedha wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Matungulu akiwa na mkewe wakifuatilia Ibada.
Mtoto wa Kwanza wa marehemu, Alex Bashonga ambaye anaishi Canada akisoma wasifu wa marehemu.
Mtoto wa marehemu wa mwisho, Toussaint Bashonga akimwelezea mama yake.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia Ibada.
Kutoka kushoto ni Toussaint, Bashonga, Darius Bashonga, Lucien Bashonga, Yves Bashonga ambao wanaishi Maryland na Kaka yao Alex Bashonga anayeishi Canada katika picha ya pamoja baada ya Ibada ya kumuombea mpendwa mama yao kumalizika.
Familia ya Bashonga katika picha ya pamoja akiwemo mdogo wao wa kike (aliyevaa nguo nyeupe mstari wa nyuma katikati) anayeitwa Alexandrine Bashonga.
Alice Mkabane akimpa mkono wa pole Yves Bashonga.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment