|
Mshiriki wa shindano la BBA kutoka nchini Tanzania Mwisho Mwampamba amevamiwa na polisi hivi karibuni nyumbani kwake huku wakimtaka arudi kwao. |
|
Mwisho aliandika kupitia mtandao wa facebook akilalamika jinsi polisi hao walivyomnyanyasa na kusema kuwa Namibia ni nchi huru na kila mtu ana haki ya kuishi. |
|
Mwisho amekuwa akiishi na familia yake nchini humo kwa miaka kadhaa baada ya kufunga ndoa na aliyekuwa mshiriki mwenzake wa BBA Meryl Shikwambane na kubahatika kupata watoto wawili. |
|
Mwisho Mwampamba pia,amesikitishwa na vitendo vya ubaguzi alivyofanyiwa na Polisi wa nchini Namibia, anakoishi na mkewe, Meryl Shikwambane. |
|
Akiandika kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, akisema nchi hiyo sasa hivi imekuwa kama Afrika Kusini, ambako wageni, hasa wenye ngozi ya Kiafrika, hupata shida ya kuishi kutokana na kubaguliwa. |
|
“Mimi nimeoa mtu wao na nimezaa naye mtoto, nashangaa kubaguliwa na polisi hao, pia inashangaza kuona wakiwahudumia vyema wageni kutoka barani Ulaya, lakini sisi Waafrika wenzao tunabaguliwa,” alisema |
Mwampamba.
Mkali huyo ameshangazwa kupewa hati ya kuishi nchini humo kwa miezi miwili pekee, wakati ameoa mwanamke wa
nchi hiyo, huku akipata shida hiyo hata mipakani.
No comments:
Post a Comment